Dar kuwa na awamu sita za mradi wa mabasi yaendayo kasi, Serikali yaliambia Bunge

Awamu ya pili ambayo tayari fedha zake zimeidhinishwa inatarajia kuanzia Kariakoo hadi Mbagala wilayani Temeke

Dar kuwa na awamu sita za mradi wa mabasi yaendayo kasi, Serikali yaliambia Bunge

Awamu ya pili ambayo tayari fedha zake zimeidhinishwa inatarajia kuanzia Kariakoo hadi Mbagala wilayani Temeke

11 May 2018 Friday 13:46
Dar kuwa na awamu sita za mradi wa mabasi yaendayo kasi, Serikali yaliambia Bunge

Na Mwandishi Wetu

KATIKA kuondoa tatizo la foleni jijini Dar es Salam serikali imesema kuwa itakuwa na awamu sita za mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART), Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaam Josephat Kandege amesema.

Alikuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Ilala Musa Zungu (CCM) aliyetaka kujua mikakati ya serikali katika kuiokoa wilaya ya Ilala ambayo imekuwa ikipokea magari kutoka sehemu zote za nchi.

Hata hivyo Naibu Waziri huyo hakufafanua awamu hizo zitahusu maeneo au wilaya gani, lakini awamu ya Kwanza ambao imeanza kufanya kazi ni ile ya mabasi kutoka kimara hadi Mbezi na Morocco hadi Kariakoo.

Inatarajiwa kuwa awamu ya pili ambayo tayari fedha zake zimeidhinishwa inatarajia kuanzia Kariakoo hadi Mbagala wilayani Temeke.

Akijbu swali hilo, Naibu Waziri Kandege alisema kuwa awamu ya kwanza na ya pili ya mradi wa mabasi yaendayo kasi umefanya vizuri na wananchi wengi wanaunga mkono.

Alisema kuwa ni azma ya serikali kuwa na miradi kama hiyo ipatayo sita   kwa lengo la kuondoa msongano wa magari kabisa katika jiji la Dar es Salaam.

Alidokeza pia serikali imekuwa ikiendelea kushughulikia tatizo la barabara za jimbo la Segerea kwa kutenga zaidi ya shilingi milionii 800.

Alisema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kujenga kiwango cha changarawe baadhi ya barabara katika jimbo hilo kwa kipindi cha mwaka huu wa fedha. 

Akijibu swali la Mbunge wa Mbeya Vijijini, Oran Njeza (CCM) aliyetaka kujua lini serikali itajenga bandari kavu eneo la Inyala, Naibu waziri wa Tamisemi Elias Kwandikwa alisema kuwa tayari maandalizi yameanza.

Alieleza kuwa kiasi cha ekari 108 kimekwisha tengwa kwa ajili ya ujenzi wa bandari hiyo na kwa sasa tathmini itafanyika kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi waliopisha ujenzi wa mradi huo.

Kuhusu ajali mbali mbali, Naibu Waziri Kwandikwa aliwataka wadau wote ikiwemo wananchi kushirikiana na serikali kuzipunguza au kuondoa kabisa.

Alisema kuwa serikali intambua tatizo hilo na kuwa itaendelea kutoa elimu kwa wadau  wa usafiri ili wavitumie vyombo vyao vizuri.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.