Dk Mwanjelwa ampongeza Zitto kwa kuuliza swali zuri bungeni

Awali mbunge huyo alisema kuwa Februari mwaka jana kamati ya maendeleo ya Mkoa RCC ilipitisha mkakati wa kuendeleza zao la mchikichi wizarani lakini hadi...

Dk Mwanjelwa ampongeza Zitto kwa kuuliza swali zuri bungeni

Awali mbunge huyo alisema kuwa Februari mwaka jana kamati ya maendeleo ya Mkoa RCC ilipitisha mkakati wa kuendeleza zao la mchikichi wizarani lakini hadi...

14 June 2018 Thursday 12:20
Dk Mwanjelwa ampongeza Zitto kwa kuuliza swali zuri bungeni

Na Mwandishi Wetu

NAIBU waziri wa Kilimo , Dk Mary Mwanjelwa amempongeza Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe (ACT –Wazalendo) kwa kuuliza swali zuri na kumuomba amletee nakala ya mkakati ili waifuatile

Awali mbunge huyo alisema kuwa Februari mwaka jana kamati ya maendeleo ya Mkoa RCC ilipitisha mkakati wa kuendeleza zao la mchikichi wizarani lakini hadi leo bado hawajajibiwa.

Alisema kutojibu huko kunaweza kuthibitisha kwamba serikali imeshikwa na wafanyabiashara wa mafuta hayo ya kula wanaoagiza kutoka nje, alitaka kueleza sababu za kukaa kimya.

Akijbu , Naibu waziri Mwanjelwa alisema kuwa mbunge huyo ameuliza swali zuri na kumuomba kumpatia nakala ya mkakati huo ili wizara ifuatilie na kuifanyia kazi.

Kuhusu kusua sua kwa vituo vingi vya maendeleo ya kilimo , alisema kuwa inatokana na upatikanaji wa fedha. Aidha aliviomba vyuo vya utafiti wa kilimo kujiongeza na kutokutegemea fedha za serikali. Alisema vituo hivyo vinaweza kuandika maandiko mbali mbali kwa wafadhili kwa ajili ya kupata fedha za utafiti na maendeleo.

Updated: 14.06.2018 12:34
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.