Hakuna kigugumizi mahesabu ya ushirika kujadiliwa bungeni,asema naibu waziri

Hakuna kigugumizi mahesabu ya ushirika kujadiliwa bungeni,asema naibu waziri

31 May 2018 Thursday 15:25
Hakuna kigugumizi mahesabu ya ushirika kujadiliwa bungeni,asema naibu waziri

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema kuwa haina kigugumizi cha kuwasilisha muswada bungeni utakaofanya mahesabu ya vyama vya ushirika kupelekwa bungeni kwa ajili kujadiliwa.

Hayo yamesemwa bungeni leo na Naibu Waziri wa Kilimo Dk Mary Mwanjelwa, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Maswa magharibi Mashimba Ndaki (CCM) aliyetaka kujua sababu zinazoikwamisha serkali kuwasilisha hesabu za vyama hivyo bungeni.

Alisema kuwa bunge limechaguliwa na wananchi na kwanini serikali inaona mashaka kuleta taarifa za Coasco ili zichambuliwe na wabunge, na kuongeza kuwa kama kikwazo ni sheria basi uletwe muswada wa kuibadilisha.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Mwanjelwa aliseama kuwa Coasco ni shirika la umma ambalo lililanzishwa mwaka 1982 kwa lengo la kukagua taarifa za vyama vya ushirika.

Alisema kuwa mara baada ya ukaguzi huo, hesabu hizo hupelekwa kwenye mikutano mikuu ya vyama husika kwa ajili ya kujadiliwa na wanachama.

Hata hivyo alibainisha kuwa haina kigugumuzi kupeleka mabadiliko yatakayofanywa hesabu hizo kujadiliwa na bunge kama taasisi nyingine za serikali zinavyofanya.

Alimtoa shaka mbunge huyo kuwa serikali itaufanyia kazi ushauri wake kwa maslahi mapana ya taifa na wana ushirika.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.