banner68
banner58

Hiki ndicho kilichomwokoa mhandisi wa kivuko cha MV Nyerere

Hiki ndicho kilichomwokoa mhandisi wa kivuko cha MV Nyerere

22 September 2018 Saturday 15:31
Hiki ndicho kilichomwokoa mhandisi wa kivuko cha MV Nyerere

OIL imetajwa kuwa miongoni mwa sababu zilizookoa maisha ya Mhandisi wa Kivuko cha MV Nyerere, Alphonce Charahani, aliyeokolewa akiwa hai baada ya kupita saa 48 tangu kivuko hicho kizame katika Ziwa Viktoria.

Wakizungumza baada ya kumuokoa mhandisi huyo, asubuhi ya leo tarehe 22 Septemba 2018, baadhi ya waokoaji walisema mbinu ya Mhandisi Charahani ya kujipaka oil mwilini, ilimsaidia kuzuia maji ya ziwa hilo kuingia kwenye vinyweleo vyake.

Kivuko hicho kilizama kwenye ajali iliyotokea tarehe 20 Septemba 2018 wakati kikisafirisha abiria kutoka kisiwa cha Bugorora kwenda Kisiwa cha Ukara kwenye Ziwa Victoria.

Baada ya kuokolewa, Mhandisi Charahani alikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Busya kilichopo kisiwani Ukerewe kwa matibabu zaidi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
God 2018-09-22 23:49:58

Hamjui kuandika habari iliojitosheleza,

Avatar
YOHANA JUMA 2018-09-23 15:26:17

Mimi binafis nmeguswa namsiba wa mv nyerere mm nimzaliwa wa magu mwanza namuomba mungu awalaze mahali pema peponi amina

Avatar
Savio 2018-09-28 21:04:47

Mwandishi wa habar hana maelezo yenye ujazo dhid ya uokoz wa muhandis

Avatar
emanuel 2018-09-29 10:38:46

rest in peace all dead in.

Avatar
hyazint 2018-10-03 05:53:22

tumien taaluma zenu kuandika habar kiukamilifu