Jela maisha kwa jaribio la kumuua mkewe

Alibanwa na madeni, ataka fedha za bima za mkewe aanze maisha mapya na hawala

Jela maisha kwa jaribio la kumuua mkewe

Alibanwa na madeni, ataka fedha za bima za mkewe aanze maisha mapya na hawala

15 June 2018 Friday 16:15
Jela maisha kwa jaribio la kumuua mkewe

Sajini wa zamani wa jeshi la Uingereza ambaye alijaribu kumuua mkewe kwa kuharibu parachiti amehukumiwa kifungo cha angalau miaka 18 jela.

Mzaliwa wa Afrika Kusini Sajini Emile Cilliers alikutwa na hatia mwezi uliopita katika mashtaka mawili ya kujaribu kuua kwa kuharibu parachute na kuharibu mrija wa hewa nyumbani kwa wanandoa hao.

Victoria Cilliers alinusurika kwa kutua kwenye shamba lililolimwa baada ya kuanguka umbali wa mita 1200 mwezi Aprili 2015.

Waendesha mashtaka walisema mtuhumiwa, mwenye umri wa miaka 38 alikuwa anakabiliwa na madeni na alitaka fedha za bima za mkewe ili aweze kulipa madeni hayo na kuanza maisha mapya na mpenzi mwingine.

Cilliers alihukumiwa kifungo cha maisha jela Ijumaa katika mahakama ya Winchester Crown kusini mwa Uingereza, bila nafasi yoyote ya parole mpaka baada ya miaka 18 kupita. Jaji Nigel Sweeney alimwambia “hili lilikuwa kosa ovu lisilo na kipimo.”

Azania Post

Updated: 15.06.2018 16:19
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.