banner68
banner58

Kama wewe ni mtalamu wa kuhonga, basi leo fanya hivi

Hakuna ubishi kuwa popote katika maendeleo ya mwanaune nyuma lazima kuna mtu makini na si mwingine ni mama

Kama wewe ni mtalamu wa kuhonga, basi leo fanya hivi

Hakuna ubishi kuwa popote katika maendeleo ya mwanaune nyuma lazima kuna mtu makini na si mwingine ni mama

13 May 2018 Sunday 15:10
Kama wewe ni mtalamu wa kuhonga, basi leo fanya hivi

Na Amini Nyaungo

Umuhimu wa mama kila mmoja anafahamu wala hakuna asiyejua thamani ya mama yake. Hii kutokana na namna wazazi walivyowapa faraja katika shida na raha huku wakipata taabu kwa ajili ya watoto wao.

Hakuna ubishi kuwa popote katika maendeleo ya mwanaune nyuma lazima kuna mtu makini na si mwingine ni mama.


Anaweza akashinda njaa yeye akatamani mwanae ushibe.


Azania Post imezunguna na baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam kuelezea namna umuhimu wa Mama katika siku ya leo.


Lucy David yeye ni mkazi wa Kimara Dar es Salaam ni mtoto wa kwanza katika familia ya wazazi wake, amesema namna ambavyo anampenda mama yake hawezi simulia.


"Leo ni siku adimu kwangu, namshumuru mama amenilea katika mazingira ya furaha na taabu hakujali namna gani namsumbua bali aliweza kunijali na kunipa kila nilichokuwa nahitaji. Amenisomesha na kunipa kila kitu.


Leo hii ni siku yao natumia fursa hii kusema nampenda sana mama yangu, " amesema.


Naye Fatma Mashaka wa Ilala Dar es salaam amesema licha ya mama yake kuwa mbali na Dar es Salaam, leo atatumia muda mwigi kuongea naye ili kumueleza namna anavyompenda.


"Mama yangu yupo Dodoma ila leo nitampigia na kumwambia namna gani nampenda, baada ya Mungu basi mama anafuata ana mapenzi mema sana juu yangu, amenilea katika mazingira magumu hakujali namwambia nampenda sana,” amesema.


Kila mmoja anaweza kueleza yake juu ya umuhimu wa mama na siku muhimu ya kina mama Duniani, je wewe unanini cha kumwambia leo?


Usitumie mitandao ya kijamii kuonesha unampenda wakati hujampigia simu hata dakika moja kumueleza namna gani unampenda, kama bado chukua simu yako jaribu kumpigia umueleze namna unampenda.


Leo kama unajua kuhonga ndiyo siku muhimu kwako wewe kumuhonga mama yako kwani unapata faida mara mbili, unalipwa mema kwa Mungu pia uvazidisha upendo.

Jopo zima la Azania Post linachukua fursa hii kuwatakia heri na fanaka mama wote dunia, kwani inatambua umuhimu wao hadi kuwepo hii leo.Azania Post

Updated: 14.05.2018 15:44
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.