Kamati ya bunge yafukua makaburi, mawaziri wa zamani sasa kuchunguzwa

Alisema kuwa kamati yake imebaini madudu katika sekta hiyo ikiwamo mikataba ya serikali na wawekezaji ilivyoliingiza hasara taifa kupitia sekta hiyo huku...

Kamati ya bunge yafukua makaburi, mawaziri wa zamani sasa kuchunguzwa

Alisema kuwa kamati yake imebaini madudu katika sekta hiyo ikiwamo mikataba ya serikali na wawekezaji ilivyoliingiza hasara taifa kupitia sekta hiyo huku...

03 June 2018 Sunday 15:31
Kamati ya bunge yafukua makaburi, mawaziri wa zamani sasa kuchunguzwa

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa kamati iliyoundwa na Spika wa Bunge Job Ndugai kuchunguza mwenendo wa biashara amesema kamati yake imependekeza mikataba ambayo viongozi waandamizi wa Wizara ya nishati na madini waliingia ambayo imeitia serikali hasara ya mamilioni ya fedha kuchunguzwa

Akizungumza kutoka Dodoma mwenyekiti huyo , Dunstan Kitandula alisema wakati wa kukabidhi ripoti hiyo kuwa mawaziri wachache walioshika wizara hizo wachunguzwe.

Alisema kuwa kamati yake imebaini madudu katika sekta hiyo ikiwamo mikataba ya serikali na wawekezaji ilivyoliingiza hasara taifa kupitia sekta hiyo huku mfanyakazi mmoja akilipwa mamilioni.

Katika ripoti hiyo, Kitandula amewataja mawaziri zamani wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, Daniel Yona, Nazir Karamagi, William Ngeleja na marehemu Abdallah Kigoda kuingia mikataba hiyo, ambayo alisema imekuwa ikiliingizia hasara taifa.

“Mawaziri hao walikuwa wakisaini mikataba hiyo na makampuni ya kigeni kupitia aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Yona Kilaghane .

“Aidha, katika uchunguzi wetu, kamati ilibaini mfanyakazi mmoja wa kigeni wa Kampuni ya Payet, analipwa mshahara wa Sh milioni 96 kwa mwezi tofauti na wazawa ambao wanalipwa mshahara kidogo.

“Kutokana na hali hiyo, kamati inapendekeza vyombo vya dola vichunguze mikataba yote katika sekta ya gesi iliyoingiwa na viongozi hao ili kuona kama walikuwa na nia njema au waliiisaini kwa kujali maslahi yao binafsi.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.