Kamwelwe aziondoa hofu familia zitakazopisha ujenzi mradi wa umwagiliaji Songwe

Kamwelwe aziondoa hofu familia zitakazopisha ujenzi mradi wa umwagiliaji Songwe

06 June 2018 Wednesday 15:04
Kamwelwe aziondoa hofu familia zitakazopisha ujenzi mradi wa umwagiliaji Songwe

Na Mwandishi Wetu

TANZANIA na Malawi zimeingia mkataba wa kujenga mradi mkubwa wa umwagiliaji katika bonde la Songwe mara baada ya kupata mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Waziri wa Maji na Umwagiliaji Isack Kamwelwe alisema leo kuwa pindi tu fedha ikipatikana ujenzi wa mabwawa makubwa matatu utaanza kwa lengo la kuimarisha kilimo cha umwagiliaji.

Aliwaambia wabunge katika kipindi cha maswali na majibu kuwa mkataba huo utasainiwa baadaye mwaka huu utawezesha pia kupatikana kwa umeme na pia utazuia matumizi mabaya ya maji.

Alisema kabla ya kuanza kwa mradi huo kutakuwa na maandalizi ya awali ambapo familia zitakazoguswa zitalipwa fidia kwa mujibu wa sheria.

Aliskuwa akijibu swali la Mbunge wa Ileje, Janet Mbene (CCM) aliyetaka kujua lini mradi huo mkubwa utaanza.

Akijibu, Waziri Kamwelwe alisema kuwa serikali ipo imara na imedhamiria kumaliza miradi mbali mbali ya maji huku ikitumia watalaam mbali mbali katika sekta hiyo.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.