Khamenei atoa maagizo mazito kuhusu kurutubisha madini ya uranium

Wakati huohuo, waziri mkuu wa Israel Bw. Netanyahu anaendelea na ziara yake barani Ulaya kuwashawishi washirika wake kuitikia mwito wake wa kubadilisha makubali

Khamenei atoa maagizo mazito kuhusu kurutubisha madini ya uranium

Wakati huohuo, waziri mkuu wa Israel Bw. Netanyahu anaendelea na ziara yake barani Ulaya kuwashawishi washirika wake kuitikia mwito wake wa kubadilisha makubali

05 June 2018 Tuesday 11:22
Khamenei atoa maagizo mazito kuhusu kurutubisha madini ya uranium

Na Mwandishi Wetu

IRAN kuanza kurutubisha madini ya Uranium ambayo hutumika kutengenezea bomu la nyuklia, kinyume na makubaliano ya kimataifa.

Tayari Kiongozi mkuu wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei ameliagiza Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran AEOI kujiandaa kurutubisha madini ya Uranium.

Ametoa agizo hilo kwenye hotuba yake aliyoitoa kwenye televisheni jana ili kuadhimisha miaka 29 tangu kufariki mwasisi wa Iran Imam Khomeini. Amesema inaonekana kuwa baadhi ya serikali za Ulaya zinatarajia kuwa Iran itakubali vikwazo na kuacha shughuli za nyuklia.

Iran inafanya majadiliano na nchi za Ulaya kuhusu kuokoa makubaliano ya nyuklia ya Iran baada ya Marekani kujitoa. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Iran inaweza kurutubisha uranium katika ngazi ya asilimia 3.5.

Wakati huohuo, waziri mkuu wa Israel Bw. Benjamini Netanyahu anaendelea na ziara yake barani Ulaya kuwashawishi washirika wake kuitikia mwito wake wa kubadilisha makubaliano ya nyuklia ya Iran.

Kansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel na Bw. Netanyahu wamekubaliana kuhusu kuizuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia, lakini wana maoni tofauti katika jinsi ya kutimiza lengo hilo. Bibi Merkel ameahidi kudumisha makubaliano hayo licha ya Marekani kujitoa, ili kuizuia Iran kumiliki silaha za nyukli

Azania Post

Updated: 05.06.2018 11:58
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.