Kijana akamatwa akifukua kaburi la mama yake

Kijana huyo alisema alikuwa akitafuta mama yake kwa kuwa alikuwa anahitaji mwenza katika maisha yake

Kijana akamatwa akifukua kaburi la mama yake

Kijana huyo alisema alikuwa akitafuta mama yake kwa kuwa alikuwa anahitaji mwenza katika maisha yake

02 June 2018 Saturday 12:56
Kijana akamatwa akifukua kaburi la mama yake

Polisi nchini Kenya wanamshikilia kijana mwenye umri wa miaka 17 baada ya kukutwa kwa mara ya pili akijaribu kufukua kaburi la mama yake.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa katika kijiji cha Kamae huko Kandara akiwa na jembe zikiwa zimebaki inchi chache tu kufikia mabaki ya mama yake Lucy Njeri ambaye alizikwa miaka miwili iliyopita.

Siku ya Alhamisi, kijana huyo alitoroka kutoka kambi ya Polisi ya Ngurweini, kabla ya kukutwa kwa mara ya pili kwenye kaburi la mama yake akitafuta mwili.

Katika matukio hayo mawili, kijana huyo alisema alikuwa akitafuta mama yake kwa kuwa alikuwa anahitaji mwenza katika maisha yake.

Ndugu zake walisema walikuwa walifahamishwa kuhusu tabia za kijana huyo kabla ya kutoa taarifa kwa mamlaka husika na ambao walishindwa kutoa shauri nasaha kwa vijana ambaye alisisitiza kwamba alikuwa akimtafuta mama yake kaburini.

Mzee Wanyoike Karuga alisema kijana huyo alichimba karibu na futi tatu kabla ya kukamatwa na wakazi wa eneo hilo waliokuwa wakipita karibu na nyumba inayoishi familia ya kijana huyo.

"Kijana ni yatima na uamuzi wake kuchimba kaburi la mama yake unashtua. Anahitaji ushauri kutoka kwa wataalam, "alisema Karuga.

Wanakijiji walifukia tena kaburi hilo huku mtuhumiwa akipelekwa kwenye Kituo cha Polisi cha Kandara kwa mahojiano.

Mkuu wa kituo cha polisi cha Kandara Wilson Kosgey alisema wameanzisha uchunguzi, ili kufahamu ni kwa nini kijana huyo ameamua kufukua kaburi la mama yake.

"Polisi bado haijamstaki mtuhumiwa kwa kuwa anaweza kuwa na matatizo ya kiakili. Alikimbia kutoka kwenye kituo cha polisi na sisi tunahisi kwamba mtuhumiwa hana akili timamu,"alisema Kosgey.

Standard Media

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.