banner68
banner58

Kisa cha mwanamke aliyekataa kuolewa na mwanaume aliyemtolea figo

Kisa cha mwanamke aliyekataa kuolewa na mwanaume aliyemtolea figo

12 July 2018 Thursday 13:03
Kisa cha mwanamke aliyekataa kuolewa na mwanaume aliyemtolea figo

Katika mahusiano kuna mambo mengi ambayo yanatokea mengi ni yale yatarajiwayo na mengine ni yale yasiyotarajiwa.

Huko London mwanaume mmoja anayejulikana kama Simon Louis (49) amekataliwa ombi lake na mpenzi wake la kumuoa Mary Emmanuella (41) ambaye ni mpenzi wake aliyempenda mpaka kuokoa maisha yake mara baada ya kujitolea figo yake kumpandikizia na kunusuru maisha yake pindi figo zake kufeli na kupoteza fahamu kwa muda wa miezi miwili.

Hata hivyo Simon alipohojiwa na chombo cha habari cha Metro UK alisema kuwa hajutii maamuzi yake ya kumpa figo mwanamke huyo aliyempenda hata mara baada ya kukataa ombi lake alipopona ugonjwa uliokuwa unamsumbua wa figo.

“Nilimpa moyo wangu, lakini pia nilijifikiria nikampa na figo yangu, chochote kilichotokea sijutii wala sitojutia kwa kumpa zawadi ya maisha,” amesema Simon.

Aidha Mary Emmanuella amesema ataendelea kuwa rafiki wa karibu wa Simon.

Ni rafiki yangu sana na daima itakuwa hivyo, mapenzi kati yetu ni ya kweli, Simon angefariki kwa kile alichokifanya kwa ajili yangu,” amesema Simon.

Kwa mara ya kwanza wapenzi hao walikutana Club mnamo mwaka 1990 pindi Simon akiwa na umri wa miaka 28 huku Mary akiwa na umri wa miaka 20.

Mnamo Septemba 2014 Mary akiwa na miaka 37, gafla alianguka na ngozi yake kugeuka kuwa njano, mwanae Dwayne alimkuta chini akiwa anatapika na kumkimbiza hospitali huko London ambapo alikutwa na ugonjwa wa figo uliofikia hatua mbaya na njia pekee kuokoa maisha yake ilikuwa ni kupandikiza figo nyingine.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.