Magufuli ashtushwa na kifo cha wanafunzi wawili chuo kikuu Iringa leo

Mwaka jana, walijiunga na chuo kikuu cha Ruaha Catholic University na kuanza na masomo ya kompyuta kabla ya kuanza masomo kamili Oktoba.

03 June 2018 Sunday 12:19
Magufuli ashtushwa na kifo cha wanafunzi wawili chuo kikuu Iringa leo

Na Mwandishi Wetu

WANAFUNZI wawili wa Chuo Kikuu cha Ruaha Catholic cha mkoani Iringa wamefariki leo asubuhi katika hospitali ya mkoa huo.

Taarifa zinasema Maria na Consolata pacha waliozaliwa wakiwa wameungana wamefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kifo chao kimewagusa wengi Tanzania, wengi wakituma salamu zao za rambirambi kupitia mitandao ya kijamii.

Rais Dkt John Magufuli, ambaye miezi kadha alikutana na pacha hao, ameeleza kusiktiishwa kwake na vifo vyao.

Pacha hao waliozaliwa miaka 20 iliyopita wamekuwa wakitunza na watawa wa kanisa Katoliki tangu baada ya kuzaliwa.

Mwaka jana, walijiunga na chuo kikuu cha Ruaha Catholic University na kuanza na masomo ya kompyuta kabla ya kuanza masomo kamili Oktoba.

Maria na Consolata walikuwa wamefanya mitihani yao ya mwisho ya kidato cha sita, katika shule ya Sekondari ya Udzungwa mjini Iringa, Kusini magharibi mwa Tanzania na kufaulu.

Wakati huo, walieleza furaha yao kuu baada ya kufaulu mtihani na kueleza ndoto zao.

"Tulipokea matokeo yetu tukiwa kwenye mazingira ya nyumbani tu, tukiendelea na shughuli zetu za kila siku, tukaambiwa matokeo yametoka na tumefanya vizuri, tulikuwa tukiwaza kabla ya hapo, unajua kwenye mitihani ya mwisho huwezi kujiamini sana," alikaririwa Consolata.

Walieleza sababu za kuchagua chuo cha Ruaha kwenye mkoa waliokuwa wanaishi tofauti na vyuo vingine au kama ilivyo kwa wanafunzi wengine ambao hupenda kubadili mazingira.

Maria na Consolata walikuwa wamewahimiza wazazi kuwajibika ipasavyo kwa watoto wao wenye ulemavu wakisema hakuna lisilowezekana.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.