Maji Ziwa Rukwa hayafai kwa matumizi ya binadamu, Bunge laambiwa

Maji Ziwa Rukwa hayafai kwa matumizi ya binadamu, Bunge laambiwa

14 June 2018 Thursday 12:48
Maji Ziwa Rukwa hayafai kwa matumizi ya binadamu, Bunge laambiwa

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imethibitisha kuwa maji ya Ziwa Rukwa hayafai kwa matumizi ya binadamu, Waziri mwenye dhamana, Isaac Kamwelwe amesema bungeni leo.

Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Aida Kenani (CCM) aliyetaka kujua sababu zinazoizua serikali kutounganisha maji ya ziwa hilo na kuwapatia wananchi jirani.

Akijibu Waziri Kamwelwe alisema kuwa kamwe serikali haiwezi kuunganisha maji ya Ziwa Rukwa kwani hayafai kwa matumizi ya binadamu.

Lakini alibainisha kuwa maji ya Ziwa Tanganyika yanafaa kwa matumizi ya binadamu na sasa wizara inaandika andiko kwa ajili ya kusambaza mikoa jirani.

Kuhusu upatikanaji wa maji katika mkoa wa Rukwa, alisema kuwa kwa sasa ni asilimia mia moja na hivi karibuni Rais John Magufuli atazindua mradi mkubwa wa maji mkoani humo.

Akielezea kuondoa madini ya floride kwenye maji, alisema kuwa mpango huo upo  na kwasasa  utafanyika katika   mikoa mipya iliyobainika ambayo ni  Shinyanga Mbeya, na ule wa Arusha ambako kuna tatizo sugu kwa miaka mingi.

Aidha aliwataka wananchi wa Mbagala jijini Dar es Salaam kukaa mkao wa kula kwani serikali imesaini mkataba na kampuni moja kutoka nchini Ufaransa kwa ajili ya kuwapatia maji. Alisema kuwa kwa kipindi cha muda mfupi ujao, mkoa huo utakuwa na maji ya uhakika.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.