banner68
banner58

Majibu ya Nyalandu baada ya kuambiwa arudishe Twiga

Majibu ya Nyalandu baada ya kuambiwa arudishe Twiga

17 July 2018 Tuesday 10:59
Majibu ya Nyalandu baada ya kuambiwa arudishe Twiga

Waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii kwenye Serikali ya awamu ya nne Tanzania Lazaro Nyalandu ameingia tena kwenye headline, wakati huu ni baada ya kuambiwa arudishe Twiga.

Ilianzia pale Nyalandu alipoandika maneno ya kutia moyo, “Ukweli katika maisha ni huu, kwamba MUNGU hakuachi. Amini katika UWEZO na UKUU wake. Ujapopita katika changamoto zozote katika MAISHA, hata wale wa karibu nawe wakikuacha, Yeye ni AMINI na KWELI, HATAKUACHA, atakupigania, na atakufanya HERI kwa ajili ya UTUKUFU wake. #AMINIDAIMA”

Baada ya kuandika maneno hayo mmoja wa Followers kwenye mtandao huo wa Twitter alimjibu kwa kuandika “Ukirudisha Twiga tutakuelewa” ndipo Nyalandu akamjibu kama inavyosomeka hapa chini.

“Watu kama wewe wamelaaniwa. Huwezi kuanza siku kwa kusema UONGO ili ujisikie umesomeka kwenye mitandao ya kijamii. Ni TWIGA yupi unayetaka nimrudishe, na nilimchukua WAPI. Imeandikwa, WAONGO wote, sehemu yao ni katika ZIWA liwakalo kwa KIBERITI."

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Mzee mwamba 2018-07-17 11:31:45

Safi sana kwani kama wanataka kukudhalilisha kwa ukatili wao mungu atatenda katika uungu wake

Avatar
Ben riu 2018-07-17 13:49:59

Wenye hekima ujibu kwa hekima na wale waliotumwa uishi maisha mafupi?