Mama, binti zake wamuua baba kwa kuwakataza kuvaa ‘jeans’

Waajiri wauaji ili kummaliza mwanaume ndani ya nyumba yao

Mama, binti zake wamuua baba kwa kuwakataza kuvaa ‘jeans’

Waajiri wauaji ili kummaliza mwanaume ndani ya nyumba yao

09 July 2018 Monday 10:08
Mama, binti zake wamuua baba kwa kuwakataza kuvaa ‘jeans’

Mwanamke mmoja nchini India na binti zake wanne wamekiri kulipa wauaji ili kumuua mume / baba yao aliuawa kwa sababu alikataa kuwaruhusu kuvaa mavazi aina ya ‘jeans’.

Mwili wa Meharbaan Ali, inspekta msaidizi wa polisi, ulipatikana katika mfereji wa maji taka huko Shahjahanpur, Uttar Pradesh, kmita 250 tu kutoka nyumbani kwake, siku ya Jumapili.

Uchunguzi ulianza na haikuchukua muda mrefu kwa polisi wa eneo hilo kujua kwamba familia ya mtu huyo inaweza kuwa ilishiriki katika mauaji yake.

Kamera zilizowekwa katika eneo hilo na uthibitisho kamili wa historia ya miito ya simu ya kila mwanachama wa familia iliwasaidia wapelelezi kupata mwanga juu ya kesi hiyo na hatimaye mke na mabinti hao kukiri.

"Kutoka wakati mwili wa Ali ulipatikana, tulihisi kuhusika kwa familia, kwa sababu mwili ulipatikana mita 250 tu kutoka nyumba zao," Daya Chand Sharma, Mkaguzi wa polisi wa Sadar Bazaar, alisema. "Tulichukua kumbukumbu za kina za miito ya simu ya watu wote wa familia na tukagundua kuwa mke wa Ali, Zahida, alikuwa akiita nambari fulani mara kwa mara."

Baada ya kuchunguza picha za CCTV zilizowekwa katika eneo la karibu na nyumba ya Ali, polisi waligundua kwamba mtu aliyeuawa amefika nyumbani karibu 04:45 asubuhi, baada ya kuondoka kituo cha polisi saa 4.

Wauaji waliojulikana tu kwa majina ya Tahseen na Ehsaan wanaweza kuonekana wakiingia ndani ya nyumba muda mfupi baada ya hapo. Jioni hiyo hiyo, wanawake hao watano waliwasaidia wauaji wawili kubeba mwili wa Ali kwenye pikipiki ili uweze kutupwa katika mfereji wa karibu.

Kwa ushahidi wazi wa ushirikishwaji wao, Zahida na binti zake wanne hawakuwa na cha ziada bali kukiri juu ya kupanga njama ya mauaji hayo. Wanawake watano waliripotiwa kuwalipa Tahseen na Ehsaan $ 1,450 (Sh 3,298,000) ili kumuua Ali, wakiwalipa nusu kabla na iliyobaki baada ya kazi hiyo kukamilika.

Inspekta Daya Chand Sharma aliwaambia waandishi wa habari kwamba wakati wa kukiri kwao, mke na binti walisema kuwa walikasirishwa na Ali kwa sababu ya vikwazo vikali alivyowawekea, ikiwa ni pamoja na kuwazuia kuvaa ‘jeans’.

Hata hivyo watapata zaidi ya uhuru baada ya kuondoka kwa Ali. Kama mjane, Zahida angepata pia nusu mshahara wa mumewe kama pensheni, pamoja na fedha za ziada ambazo wanategemezi wa polisi hupata baada ya kufariki. Mmoja wa binti za Ali pia alitumaini kwamba atachukua kazi yake kwenye kituo cha polisi.

Zahida Begum, 52, na binti zake Saba, 26, Zeenat, 22, Iram, 19, na Alia, 18 walikamatwa na wauaji wawili bado hawajatiwa nguvuni.

Keywords:
MauajiIndia
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.