Mbunge CUF amfagilia Rais Magufuli

Mbunge CUF amfagilia Rais Magufuli

31 May 2018 Thursday 15:17
Mbunge CUF amfagilia Rais Magufuli

Na Mwandishi Wetu

WABUNGE wawili mmoja wa Chama Cha wananchi (CUF) na mwingine wa Chama Cha Mapinduzi wamempongeza Rais John Magufuli kwa jiitihada zake kwa kuhakikisha riba zinazotolewa na benki za kibiashara zinashuka ili wananchi wengi waweze kuchukua mikopo.

Akizungumza katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni Dodoma leo, Mbunge wa Konde Hatibu Haji (CUF) alisema kuwa anampongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kusimamia mabenki kupungza riba.

Aliseam kuwa ni kweli benki ya CRDB imekuwa ya kwanza kushusha riba na kuitaka serikali kueleza lini itachukua hatua za kisera kusimamia suala hilo kwa manufaa ya taifa.

Naye Mbunge wa viti Maalum Munde Tambwe (CCM) alimpongeza pia Rais Magufuli lakini akazigeukia taasisi kama FINCA na PRiDE Tanzania kwa kutoza riba ya hadi asilimia 33 na kuitaka serikali kueleza mikakati yake kupunguza.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji alisema kuwa biashara ya fedha ni huria.

Alisema kuwa gharama za benki zinaamuliwa na nguvu ya soko na serikali haina mamlaka ya kuzilazimisha kupunguza riba hizo, lakini imekuwa ikichukua hatua za kisera ili kupunguza.

Alisema hatua hizo ni pamoja na kuzitaka taasisi za kifedha (mabenki) kutoa taarifa zao za kifedha Benki Kuu ya Tanzania, na kuwa benki hiyo imepunguza kiwango cha riba inachotoza taasisi za kifedha kutoka asilimia 19 hadi 9.

Alidokeza kuwa baada ya baadhi ya hatua za kisera kuchukuliwa kuna benki kadhaa zimeanza kupunguza riba.

Alisisitiza kuwa serikali itaendelea kuchukua hatua hizo ili kuyafanya mabenki kupunguza riba.

Aliongeza kuwa kwa kutambua umuhimu wa wajasiriamali wadogo serikali imezindua sera ya huduma ndogo za fedha mwaka jana.

Alifafanua kuwa serikali pia inatunga sheria maalum kwa ajili ya kuwalinda wajasiriamali wadogo na hasa wakopaji ili wasiumizwe sana.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.