Mchakato wa kuhamisha stendi ya mabasi kutoka Mbagala kuelekea Vikindu waanza

Alisema kuwa wazo la kujenga stendi hiyo ya kisasa lilitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Alisema kuwa Waziri Mkuu alipendekezwa kuhamishwa kwa stendi ya...

Mchakato wa kuhamisha stendi ya mabasi kutoka Mbagala kuelekea Vikindu waanza

Alisema kuwa wazo la kujenga stendi hiyo ya kisasa lilitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Alisema kuwa Waziri Mkuu alipendekezwa kuhamishwa kwa stendi ya...

13 June 2018 Wednesday 09:31
Mchakato wa kuhamisha stendi ya mabasi kutoka Mbagala kuelekea Vikindu waanza

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imeanza kuchukua hatua kupunguza foleni kubwa eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam kwa kuhamisha stendi ya mabasi ya mikoani na kujenga nyingine kubwa ya kisasa eneo la Vikindu mkoani Pwani.

Akizungumza kwenye mahojiano na Azania Post Mkuu wa Mkoa wa Pwani Evarist Ndikilo, alisema kuwa tayari eneo la ekari 50 kwa ajili ya ujenzi wa stendi hiyo ya kisasa ya mabasi aina zote limepatikana.

Alisema kuwa wazo la kujenga stendi hiyo ya kisasa lilitolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Alisema kuwa Waziri Mkuu alipendekezwa kuhamishwa kwa stendi ya Mbagala ambayo kwa sasa imezidiwa na kupelekwa eneo la Vikindu.

Ndikilo alisema kuwa tayari michoro kwa ajili ya ujenzi wa stendi hiyo mpya ya kisasa imekamilika na kuiomba halmashauri ya wilaya kuharakisha mchakato wa upatikanaji wa fedha.

Alisema kuwa halmashauri imeandika andiko kwenye taasisi moja ya kifedha kwa ajili ya kuomba mkopo wa shilingi bilioni 6 zitakazotumika kwa ajili ya ujenzi huo.

Azania Post

Updated: 13.06.2018 09:39
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.