Mgomo wamalizika, hakuna bure tena kwa mabasi yaendayo haraka

Awali abiria wa mabasi hayo, walijikuta wakipanda bure kutokana na kudaiwa kuwepo kwa hitilafu katika mfumo wa tiketi

Mgomo wamalizika, hakuna bure tena kwa mabasi yaendayo haraka

Awali abiria wa mabasi hayo, walijikuta wakipanda bure kutokana na kudaiwa kuwepo kwa hitilafu katika mfumo wa tiketi

05 June 2018 Tuesday 13:15
Mgomo wamalizika, hakuna bure tena kwa mabasi yaendayo haraka

Na Mwandishi Wetu

ABIRIA wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam (Udart) ambao wamekuwa wakisafiri bure kwa siku mbili kutokana na mgomo wa wakatisha tiketi sasa wameanza kulipa mara baada ya mambo kuwekwa sawa.

Azania Post imeshuhudia wakatisha tiketi hao wakiendelea na kazi zao kama kawaida tofauti na hapo jana ambapo hawakuwepo.

Awali abiria wa mabasi hayo, walijikuta wakipanda bure kutokana na kudaiwa kuwepo kwa hitilafu katika mfumo wa tiketi.

Madirisha ya vyumba vinavyotumika kukatia tiketi yalikuwa yamefungwa huku mabasi yakiendelea kubeba abiria kama kawaida.

Abiria wengi walionekana kufurahia kusafiri bure, hata hivyo baadhi ya wanaotumia kadi wamejikuta wakilipia usafiri huo kwa kuwa wanatumia mashine maalum za kugonga.

"Kumbe ni bure, sikujua inaniuma kama nikadai vile,"amesema abiria mmoja baada ya kugonga kadi yake.

Abiria mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Daudi Joshua amesema kupanda usafiri bure kumemfurahisha kwa kuwa anaona ni fidia ya usumbufu wa kusubiri magari hayo kwa muda mrefu.

"Huduma ya usafiri huu haitabiriki, tumekuwa tukipata usumbufu mkubwa, sasa leo sijui wanatoa ofa kusafisha makosa yao," amesema Joshua, mkazi wa Luguruni Mbezi.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.