banner68
banner58

Msiniue, msinifunge, mrembo aomba

Msiniue, msinifunge, mrembo aomba

13 July 2018 Friday 11:10
Msiniue, msinifunge, mrembo aomba

Malkia wa jela nchini Kenya ambaye amekutwa na hatia ya kumuua mpenzi wake ameiomba mahakama nchini humo kunusuru maisha yake, akisema kwamba amebadilika na anajutia kosa lake.

Ruth Kamande, Miss wa gereza la Lang’ata, alikutwa na hatia ya kumuua rafiki yake wa kiume, Farid Mohammed, mnamo Septemba 20, 2015.

Kupitia kwa mwanasheria wake Joynor Okonjo, Kamande alimwambia jaji kwamba yeye ni tumaini pekee la mama yake ambaye anazeeka na uzoefu wake gerezani kwa miaka miwili iliyopita umembadili na kumfanya kuwa mtu mwema Zaidi.

Kamande alikuwa akiwasilisha utetezi wake wa mwisho mbele ya Jaji Jessie Lesiit.

Wakati akitoa hukumu yake, jaji alisema kwamba Kamande alikuwa na nia mbaya wakati alipomchoma kisu Mohammed mara 22 na kumsababishia maumivu makali kutokana na ukweli kwamba majeraha hayo hayakutokea kwa mara moja, ila kwa muda.

Katika utetezi wake, Kamande alisema kwamba mpenzi wake huyo alimbaka, akifahamu kwamba alikuwa ameambukizwa virusi vya ukimwi, na kwama alijaribu kumuua.

“Anatokea nyumba ya mzazi mmoja wa kike ambaye sasa ataathirika Zaidi baada ya mwanae wa kiume kufariki. Kamande, ni mtoto pekee na tumaini la pekee kwa mama yake. Ndiyo maana anaomba umpe adhabu ndogo tofauti na hukumu ya kifo,” alisema Okonjo.

Lakini familia ya Mohammed, kupitia mwanasheria wa serikali Everline Ohunga, ilisisitiza kwamba Kamande anastahili adhabu kali. “Familia inahisi kwamba tabia yake wakati wa kesi haionyeshi mtu ambaye ana majuto. Wana uchungu kutokana namna kaka yao alivyouawa,” alisema Onunga.

Jaji Lesiit atatoa hukumu mnamo Julai 19.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.