Mtoto amwua baba yake kwa kumtukana mama

Ni mwanafunzi wa kidato cha pili

Mtoto amwua baba yake kwa kumtukana mama

Ni mwanafunzi wa kidato cha pili

13 June 2018 Wednesday 18:30
Mtoto amwua baba yake kwa kumtukana mama

Mvulana mwenye umri wa miaka 17 anayeshutumiwa kumwua baba yake baada ya baba huyo kumtukana mama yake hajaweza kujibu tuhuma hizo mahakamani akisubiri mwanasheria wa kumtetea.

Mwanafunzi huyo wa kidato cha pili katika shule ya kijiji cha Nambacha, huko Subakho nchini Kenya anadai kuwa alimwua baba yake kwa kujaribu kuifukuza familia kwenye nyumba yao Desemba 12, 2017.

Kwa mujibu wa nyaraka za matibabu, marehemu alipigwa kwa fimbo kwenye kifua na paji la uso na kusababisha kutokwa damu nyingi.

Anasemekana alirudi nyumbani akiwa amelawa na kuanza kutukana familia bila sababu ya msingi.

Katika maelezo yake, mtoto alijaribu kuingilia kati kumwomba baba yake kupunguza sauti yake lakini alimtishia kumchapa kwa fimbo.

"Nilikuwa nimetoka sokoni na kmkuta baba yangu akigombana na mama yangu na ndugu zangu. Nilimwomba apunguze sauti yake kwa kuwa ilikuwa kubwa sana na inasumbua amani kwa majirani. Yeye akanigeukia kwangu na kunishambulia, "alisema kijana wa kidato cha pili maelezo yake.

Mtoto anasema kwamba mara mbili alijaribu kumkwepa baba yake kabla ya kuchukua fimbo nyingine na kuitumia kumpiga baba yake ambaye aliaanguka huku damu nyingi ikimtoka.

Anasisitiza kwamba alikuwa anajaribu kujilinda mwenyewe na familia kutoka kwa baba yao ambaye alikuwa na tabia ya kumtukana mama yao na watoto wengine wakati wowote alipokuwa amelawa.

Mtoto huyo ambaye ni wa tatu kuzaliwa anashikiliwa katika Jela ya Watoto ya Kakamega na anasisitiza kuwa hakuwa na nia za kumwua baba yake aliyekuwa na umri wa miaka 60.

Kwa mujibu wa ripoti ya daktari, muathiria alikufa kutokana na majeraha kwenye tishu laini.

Anasema alishtuka sana alipoona kuwa marehemu hakuwa akipumua alipoanguka.

Azania Post

Keywords:
Kenya
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.