Mwalimu atetea wanakwaya wa kike kucheza utupu

Iliripotiwa kuwa densi ya 'utupu' ya kundi moja la kwaya ya shule nchini Afrika Kusini imevutia hisia za uchunguzi

Mwalimu atetea wanakwaya wa kike kucheza utupu

Iliripotiwa kuwa densi ya 'utupu' ya kundi moja la kwaya ya shule nchini Afrika Kusini imevutia hisia za uchunguzi

01 June 2018 Friday 11:14
Mwalimu atetea wanakwaya wa kike kucheza utupu

Na Mwandishi Wetu

KIONGOZI Wa kikundi cha kwaya ya shule huko Afrika kusini ametetea waimbaji wake kuimba wakiwa watupu huku akisema kuwa ni fahari kubwa kufanya hivyo.

Taarifa zinasema kuwa, mwalimu huyo ambaye hakutajwa alisema: Ni fahari kubwa kucheza densi ya kitamaduni ya Xhosa. Tunafurahia 'inkciyo'. Ni fahari kubwa kwa wanawake na wasichana wa Xhosa.

Iliripotiwa kuwa densi ya 'utupu' ya kundi moja la kwaya ya shule nchini Afrika Kusini imevutia hisia za uchunguzi kufanywa kutoka kwa waziri wa elimu nchini humo.

Angie Motshekga alisema kuwa alisikitika baada ya kuona kanda ya video ya wasichana hao wa Xhosa wakicheza densi yao huku wakiwa wamevalia nguo inayojulikana kama "inkciyo".

Waziri huyo wa elimu ya msingi alisema kuwa ni ukosefu wa heshima kwenda kinyume na maadili ya tamaduni za taifa hilo.

Kabila la Xhosa ndilo kabila la pili kwa ukubwa nchini Afrika Kusini.

Picha za densi hiyo katika mashindano huko Mthatha, mashariki mwa Cape, zilionekana mapema wiki hii, zikiwaonyesha wasichana hao wakicheza densi huku vifua vyao na makalio yakiwa wazi.

Kanda hiyo ya video ilipigwa wakati wa sehemu ya tamaduni ya Xhosa kulingana na mtandao wa Afrika Kusini wa Timeslive.

"Ni makosa makubwa sana kwa baadhi ya walimu ambao wanafaa kujua zaidi ya kuwanyanyasa wasichana wadogo'', chombo cha habari cha AFP kilimnukuu akisema katika taarifa.

“Hakuna makosa kupenda tamaduni na urathi wako, lakini hakukuwa na haja yoyote kucheza densi wakiwa utupu”.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.