banner68
banner58

Mwanamke ahukumiwa miaka 15 jela kwa kumbaka mvulana wa miaka 16

Mvulana alikuwa akiishi na mwanamke huyo nyumbani kwake

Mwanamke ahukumiwa miaka 15 jela kwa kumbaka mvulana wa miaka 16

Mvulana alikuwa akiishi na mwanamke huyo nyumbani kwake

23 May 2018 Wednesday 13:43
Mwanamke ahukumiwa miaka 15 jela kwa kumbaka mvulana wa miaka 16

Judith Wandera, mwenye umri wa miaka 24, amefungwa kwa miaka 15 na Mahakama huko mjini Kisumu nchini Kenya, baada ya kupatikana na hatia ya ‘kumnajisi’ mvulana mwenye umri wa miaka 16.

Wandera alishutumiwa kumnajisi mvulana mdogo katika siku mbalimbali na mashahidi waliokuwa wanaongozwa na upande wa mashtaka walimwelekezea kidole mwanamke huyo.

Nyakundi Mukaya aliiambia mahakama kuwa ushahidi wa matibabu kutoka kwa vielelezo zilizokusanywa kutoka kwa wawili hao alithibitisha kwamba mwanamke na mwanafunzi wa shule walikuwa na uhusiano wa kimapenzi.

Alibainisha kwamba kijana alikuwa akiishi nyumba moja na mtuhumiwa kwa zaidi ya miezi minne.

Mahakama hiyo iliambiwa kwamba, kutokana na jambo hili, kijana huyo aliamua kuacha shule na kuhamia nyumbani kwa mtuhumiwa kabla ya kijana huyo kuokolewa na polisi "Mvulana huyo aliokolewa Julai 7, 2017, na mshtakiwa alikamatwa na polisi," alisema Mukaya.

Baada ya kuwaokoa, alisema, kijana huyo alipelekwa kwenye kituo cha marekebisho ya tabia na baadae kurejeshwa kwa wazazi wake.

Wazazi wa mvulana aliiambia mahakamani kuwa mtoto wao aliacha kusoma baada ya kukutana na mwanamke huyo na walitafuta msaada wa polisi baada ya kijana kuamua kuanza kuishi naye.

Lakini katika utetezi wake, Wandera alisema kuwa hakujua kwamba mvulana huyo alikuwa mdogo akiongeza kwamba alikuwa ni muathirika wa madawa ya kulevya wakati walipokutana.

"Tulikutana kwenye sehemu ya baa jioni moja ya Aprili 2016 huko Kondele ambako alininunulia vinywaji. Tulibadilishana namba za simu na tukaanza kuwa wapenzi, " Wandera aliongeza kuwa hakuweza kufahamu moja kwa moja umri wa mvulana huyo kwa sababu alikuwa pia ni dereva wa boda boda na alionekana" mdogo wakati alipokuja kutoa ushahidi ".

"Alikuwa na dreadlocks wakati tulipokutana na alionekana kuwa mdogo baada ya dreadlocks zake kunyolewa kabla ya kupelekwa mahakamani kutoa mshahidi," alisema Wandera katika utetezi wake.

Standard Media

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Israel mwinami 2018-05-23 14:57:03

0675389482