Mwenyekiti CCM aeleza unafiki uliojaa kuhusiana na msiba wa mapacha walioungana

Alisema kuwa wananchi hao wajiulize waliwafanyia nini watoto hao walipokuwa wanazaliwa pale hospitali ya Ikonda iliyopo Makete au shule ya msingi na...

Mwenyekiti CCM aeleza unafiki uliojaa kuhusiana na msiba wa mapacha walioungana

Alisema kuwa wananchi hao wajiulize waliwafanyia nini watoto hao walipokuwa wanazaliwa pale hospitali ya Ikonda iliyopo Makete au shule ya msingi na...

06 June 2018 Wednesday 13:25
Mwenyekiti CCM aeleza unafiki uliojaa kuhusiana na msiba wa mapacha walioungana

Na Mwandishi Wetu

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa Albert Chalamila amewataka wananchi kuacha unafiki kuhusiana na msiba wa watoto mapacha ( Maria na Consolata) walioungana ambao wamefariki dunia juzi.

Akizungumza wakati wa misa ya mazishi ya watoto hao inayofanyika huko Tosamanga mchana huu, Mwenyekiti huyo alisema kuwa amesikitishwa sana na unafiki wa binadamu.

Alisema kuwa kama Maria na Consolata wangeamka na kuulizwa kama wanawafahamu watu wote waliohudhuria mazishi hayo wangesema kuwa hawawafahamu

Alisema kuwa wananchi hao wajiulize waliwafanyia nini watoto hao walipokuwa wanazaliwa pale hospitali ya Ikonda iliyopo Makete au shule ya msingi na sekondari hata chuo.

Alisema kuwa: “Huu ni unafiki wa nafsi zetu yawezekana wapo baadhi ya ndugu waliwakataa na leo wanajitokeza na kusema ni watoto wao”

Aliwapongeza Masista wa Kanisa Katoliki huko Ikonda kwa kukubali kuwalea tokea wakiwa watoto na kuitaka jamii kuiga mfano huo.

Aidha Mwenyekiti huyo alikishukuru pia chuo kikuu cha Ruaha Catholic kwa kukubali kuwadahili bila kujali hali zao.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela, alisema kuwa watoto hao waliamua wenyewe kuzikwa huko Tosamaganga endapo watafariki.

Alisema kuwa walikuja ndugu zao kutoka Bukoba, Makete na Mbeya wakitaka kuchukua msiba na kuwazika kwao, lakini serikali imeamua kuyazingatia maagizo yao na hivyo kuzikwa Tosamaganga mjini Iringa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.