Mzee wa kanisa asakwa kwa kumbaka mtoto wa miaka 13

Mtuhumiwa amekimbia, bado anatafutwa na polisi

Mzee wa kanisa asakwa kwa kumbaka mtoto wa miaka 13

Mtuhumiwa amekimbia, bado anatafutwa na polisi

13 June 2018 Wednesday 14:57
Mzee wa kanisa asakwa kwa kumbaka mtoto wa miaka 13

Polisi huko Nyamira nchini Kenya wanafanya uchunguzi wa kesi ya ubakaji inayomhusisha mzee wa kanisa mwenye umri wa miaka 65 na msichana mwenye umri wa miaka 13 ambaye matatizo ya utindio wa ubongo, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Nyagokiani katika Jimbo la uchaguzi la North Mugirango.

Mtuhumiwa huyo inasemekana kuwa amekimbia kutoka nyumbani kwake baada ya jaribio la kumaliza jambo hilo nje ya mahakama kukwama.

Mtu ni mhudumu wa kanisa na jirani wa nyumba anayoishi msichana. Mtuhumiwa anasemekana kuwa alimbaka mtoto huyo mnamo Mei 29, 2018 ndani ya nyumba yake.

Anashukiwa kwamba alimdanganya msichana huyo kuingia nyumbani kwake kwa kutumia maparachichi matatu na hivyo kufanikisha tendo lake hilo ovu kabla ya kumwaga maji baridi kwenye sehemu za siri za msichana huyo.

Baada ya tukio hilo, mdogo alienda nyumbani kwao akiwa amebeba maparachichi hayo matatu, moja likiwa limeharibika. Taarifa ilipelekwa kwenye kituo cha Polisi cha Ekerenyo na kuwekwa chini ya kumbukumbu namba OB 28/04/06, siku tatu baada ya tukio hilo.

Msichana huyo alitibiwa katika hospitali ndogo ya Ekerenyo.

Katika ripoti ya mwalimu mkuu wa shule, Alice Moraa ambayo iliwashirikisha wajumbe wa Bodi ya Usimamizi wa shule, mwathirika alikuwa alisafishwa na mama yake lakini aliacha nguo kama zilivyokuwa.

Ripoti hiyo inasema kuwa mtuhumiwa amejitakasa kwa kutumia mavazi ya msichana.

Katika taarifa yake, mwalimu mkuu anasema mwanafunzi huyo aliondoka shule jioni ya siku ya tukio na kamwe hakuona kitu chochote kisichokuwa cha kawaida mpaka baba pale baba wa msichana huyo alipompigia simu Juni 2.

"Hii ni kesi mbaya kabisa katika kazi yangu kama mwalimu. Inashangaza kwamba mzee kama huyo anaweza kumharibu msichana asiye na hatia, msichana ambaye hawezi kumumiza mtu yeyote, "alisema Bi Moraa.

Baba ya mwathirika huyo alisema mke wa mtuhumiwa na wazee wengine wa kanisa walijaribu kuingilia kati ili kulimaliza suala hilo kimya kimya.

"Mke wa mtuhumiwa alinifuata akiomba kuwa tutafute njia ya kutatua suala hili. Sikuweza kufanya hivyo kwa sababu nilikuwa na maumivu makali. "

Msaidizi wa Chifu wa eneo hilo Evans Nyangweta alithibitisha kutokea kwa jambo hilo akisema familia haikuwa inataka kutoa taarifa.

Alisema ana nakala kutoka kituo cha polisi cha Ekerenyo ili mtuhumiwa akamatwe.

"Tutafanya kila linalowezekana tuweze kumkamata."

Msaidizi huyo wa chifu alithibitisha kwamba alikuwa akichunguza kesi kadhaa za unyanyasaji wa kijinsia kwa wasichana wa shule.

"Changamoto kuu imekuwa upande wa familia zilizoathiriwa ambapo wazazi wanashindwa kurekodi taarifa na polisi."

Miezi saba iliyopita, Chifu wa eneo hilo alisema alimkamata mmoja wa waathirika lakini familia ya mwathirika alikataa kutoa maelezo yake polisi hivyo kuwalazimisha kumwachia mtuhumiwa.

Katika shule ya msingi ya Nyagokiani, mwalimu mkuu ana taarifa nyingi kutoka kwa wasichana ambao wameshambuliwa kingono na watu wanaofahamika vizuri kwenye jamii katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.

Kutokana na maelezo hayo, wasichana wamewataja watu, ambao wengi wao tayari wamekwishaoa lakini wamekuwa wakijihusisha na tabia chafu kingono, kama kuomba ngono, na matendo mengine ya kingono.

"Kuna wale waliotajwa zaidi ya mara tano na wasichana wetu. Nimepeleka majina yao kwenye bodi ya shule ya Usimamizi na Chifu wa eneo hilo. Tunatarajia kitu kitafanyika ili kuzuia kesi za ubakaji tena," alielezea.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.