banner68

NEC yatangaza kata mbili mpya, yaahirisha uchaguzi kata nne

NEC yatangaza kata mbili mpya, yaahirisha uchaguzi kata nne

11 July 2018 Wednesday 12:43
NEC yatangaza kata mbili mpya, yaahirisha uchaguzi kata nne

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza uchaguzi kwenye kata mbili mpya na kuahirisha uchaguzi wa kata nyingine nne.

Mabadiliko hayo yanafanya jumla ya kata zenye uchaguzi kuwa 77 badala ya 79 zilizotangazwa awali.

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa NEC, Jaji  Semistocles Kaijage amezitaja kata hizo mpya kuwa ni Kelamfua  ya Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na Kata ya Kitaya,  Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba.

“Kwa mujibu wa Kifungu cha 13 (1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata ya Kelamfua iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Rombo na Kata ya Kitaya iliyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba,” amesema Jaji Kaijage.

Jaji Kaijage amesema kwamba nafasi zote mbili za Udiwani zimetokana na kujiuzulu kwa madiwani waliokuwa wamechaguliwa awali.

Amesema uteuzi wa wagombea udiwani utafanyika Julai 16 na kampeni zitaanza Julai 17 mpaka 11 Agosti na siku ya kupiga kura ni Agosti 12.

Jaji Kaijage amevialika vyama vya siasa, wadau wote wa uchaguzi na wananchi kwa ujumla kushiriki uchaguzi huo.

Katika hatua nyingine Jaji Kaijage ametangaza kuahirishwa kwa uteuzi wa wagombea kwenye kata tatu za Tindabuligi, Kisesa, Katumba na Mlimba.

Tume itatangaza hapo baadae tarehe nyingine za uteuzi na uchaguzi katika kata hizo.

Mwananchi

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.