Papa Francis aandika barua yenye ujumbe mkali kupinga maamuzi ya Maaskofu

Papa Francis aandika barua yenye ujumbe mkali kupinga maamuzi ya Maaskofu

06 June 2018 Wednesday 12:04
Papa Francis aandika barua yenye ujumbe mkali kupinga maamuzi ya Maaskofu

Na Mwandishi Wetu

MKUU wa Kanisa Katoliki, Papa Francis ameandika barua kwa maaskofu wa Ujerumani kuruhusu waprotestanti kushiriki komunio ya kikatoliki.

Taarifa zinadai kuwa Papa Francis amepinga uamuzi wa maaskofu hao ambao ungewawezesha Waprotestanti walioana na Wakatoliki kupata Komunyo ya Kikatoliki.

Askofu mkuu Luis Ladaria, kiongozi wa ofisi ya mafundisho ya Vatican, amemueleza mkuu wa Kongamano la Maaskofu Ujerumani, Kadinali Reinhard Marx, juu ya uamuzi wa Papa katika barua iliyochapishwa na vyombo vya habari vya Kikatoliki hapo jana.

Mnamo mwezi Februari, zaidi ya theluthi mbili ya Maaskofu 60 katika Mkutano wa Maaskofu wa Ujerumani walipiga kura ya kuunga mkono pendekezo la kuruhusu Waprotestanti waliopo katika ndoa za mchanganyiko, kupokea Komunyo ya Kikatoliki chini ya masharti yaliyoainishwa.

Mkutano huo pia ulikubaliana kuchapisha miongozo ya kutumia sheria mpya kwa makanisa ya ndani. Lakini Vatican ambayo mwanzoni ilisema haitopinga suala hilo, imebadilisha mawazo baadae Jumanne kwa kusema ni suala linalohusu Kanisa la Kikatoliki kwa jumla na haliwezi kuamuliwa na maaskofu pekee.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.