banner68
banner58

Paul Makonda: Diamond ruksa kukata viuno, wengine nitawatia ndani

Paul Makonda: Diamond ruksa kukata viuno, wengine nitawatia ndani

05 October 2018 Friday 19:29
Paul Makonda: Diamond ruksa kukata viuno, wengine nitawatia ndani

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam, Paul Makonda amesema amempa ridhaa ya kutokuoa msanii Diamond na kumtaka aendelee kuwa ‘sukari ya mioyo ya watu’ sambamba na kuweka video za kukata mauno mtandaoni kutokana na alichokifanya kwa wakazi wa Tandale.

Makonda ambaye ni mlezi wa Kampuni ya WCB inayomilikiwa na Diamond amesema kwa kazi anayofanya huenda akioa mapema itamletea shida na kwamba anahitaji muda zaidi wa kufikiria kuwasaidia Watanzania wenzake.

Amesema, “Haya mambo mkiyajua vizuri bana kwanza ukiwa msanii halafu mashabiki wako wengi wakiwa wanawake ukioa wanaweza kukimbia, utafikiri ungewaoa wote,”

Makonda amewataka wasanii wote kuiga mfano wa Diamond wa kurudi na kusaidia jamii iliyowalea.

“Kwa alichokifanya Diamond hata nikiona video yake anakata mauno wala simfanyi, kitu Ila msanii hujafanya chochote halafu unasherehekea siku yako kwa kujirekodi video unakata mauno nakuweka ndani,” amesema.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.