Polisi wasimulia jinsi ‘majambazi’ wanne walivyouawa kwa risasi baada ya msako mkali

Mkuuwa kitengo cha upelelea mkoani hapo Amedeus Tesha amesema operesheni hiyo imefanyika kwa muda wa siku tano katika mikoa ya Tabora , Kigoma,

Polisi wasimulia jinsi ‘majambazi’ wanne walivyouawa kwa risasi baada ya msako mkali

Mkuuwa kitengo cha upelelea mkoani hapo Amedeus Tesha amesema operesheni hiyo imefanyika kwa muda wa siku tano katika mikoa ya Tabora , Kigoma,

05 June 2018 Tuesday 09:31
Polisi wasimulia jinsi ‘majambazi’ wanne  walivyouawa kwa risasi baada ya msako mkali

Na Mwandishi wetu

JESHI la Polisi mkoani Shinyanga limeeleza jinsi watu wanne wanaosadikiwa kuwa ni majambazi walivyouawa mara baada ya msako wa siku kadhaa.

Akizungumza Kamanda wa polisi wa mkoa huo Simon Haule, amesema watu hao wamepoteza maisha juzi wakiwa njiani kupelekwa hospitali ya Kahama mji kufuatia majeraha waliyoyapata kwa kupigwa risasi na polisi wakati wakijaribu kutoroka baada ya kuonesha silaha zao na eneo wanalotumia kuzificha baada ya kufanya uhalifu.

Mkuuwa kitengo cha upelelea mkoani hapo Amedeus Tesha amesema operesheni hiyo imefanyika kwa muda wa siku tano katika mikoa ya Tabora , Kigoma, Shinyanga hususan wilayani Kahama ambapo mtuhumiwa aliyetajwa kwa jina la Masamali Paulo alikamatwa mkoani Kigoma na kuwataja wenzake watatu ambapo amewataka watu wanaojihusisha na ujambazi kujisalimisha na silaha zao kabla ya kukamatwa.

Watu hao walikutwa na bunduki mbili, moja ikiwa ni ya kivita aina ya AK 47 na shortgun moja iliyokatwa mtutu, bastola mbili pamoja na bomu la kutupa kwa mkono na risasi 45 zikiwa katika magazini mbili tofauti

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.