Putin aruka kikwazo dhidi ya Marekani, nchi mbali mbali

Sheria hiyo inampa rais wa Urusi madaraka ya kuzuia au kudhibiti ushirikiano na mashirika ya nchi zisizo rafiki, na mashirika ya kigeni yanaweza kuzuiwa...

Putin aruka kikwazo dhidi ya Marekani, nchi mbali mbali

Sheria hiyo inampa rais wa Urusi madaraka ya kuzuia au kudhibiti ushirikiano na mashirika ya nchi zisizo rafiki, na mashirika ya kigeni yanaweza kuzuiwa...

05 June 2018 Tuesday 09:43
Putin aruka kikwazo dhidi ya Marekani, nchi mbali mbali

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Urusi, Vladimir Putin ameanza kukabiliana na vikwazo vilivyowekwa na Marekenani na nchi nyingine ambazo si rafiki wake.

Taarifa zinasema kuwa Serikali ya Urusi imesema rais Putin amesaini muswada ambao sasa utakuwa sheria kamili, inayomruhusu kuchukua hatua kukabiliana na vikwazo vilivyowekwa na Marekani na "nchi nyingine zisizo za rafiki".

Sheria hiyo inampa rais wa Urusi madaraka ya kuzuia au kudhibiti ushirikiano na mashirika ya nchi zisizo rafiki, na mashirika ya kigeni yanaweza kuzuiwa kutoa huduma kwa serikali kuu na serikali za mitaa za Russia, kufanya biashara na mashirika ya Russia au kushiriki kwenye shughuli za ubinafsishaji wa mali za Urusi.

Hatua hiyo imekuja ili kukabiliana na vikwazo vilivyowekwa na Marekani mwezi Aprili dhidi ya watu binafsi na mashirika 38 ya Urusi, wakiwemo viongozi saba wa biashara na maofisa waandamizi 17, kwa tuhuma za kuhusika na "shughuli za hujuma" kote duniani.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.