Serikali yatangaza siku mbili za mapumziko kusherehekea Eid

Siku ya Jumatatu kuwa ya mapumziko baada ya sikukuu kuangukia mwisho wa wiki

Serikali yatangaza siku mbili za mapumziko kusherehekea Eid

Siku ya Jumatatu kuwa ya mapumziko baada ya sikukuu kuangukia mwisho wa wiki

15 June 2018 Friday 11:31
Serikali yatangaza siku mbili za mapumziko kusherehekea Eid

Na Mwandishi wetu

SERIKALI nchini Nigeria imetangaza mapumziko ya siku mbili kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitri mara baada ya kumaliza kwa mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Polisi nchini Nigeria wameimarisha hatua za kiusalama kote nchini kabla ya sikukuu ya Eid el Fitr, ambapo idadi kubwa ya watalii wanatarajiwa kutembelea na kufanya ibada kwenye vituo na bustani.

Inspekta jenerali wa polisi wa Nigeria Bw. Ibrahim Idris amethibitisha kuwa hatua hizo zinatekelezwa baada ya serikali kutangaza leo Ijumaa Juni 15 na Jumatatu tarehe 18 Juni kuwa siku za mapumziko ya kusherehekea sikukuu ya Eid, ikimaanisha kumalizika kwa mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Wakati huohuo, polisi nchini humo wamewaua wateka nyara watatu katika operesheni iliyofanyika kwenye jimbo la Taraba, kaskazini mwa nchi hiyo. Kamanda Mkuu wa polisi wa Taraba Bw. David Akinremi amesema watu hao wamewateka nyara watu wengi na kuwashikilia kwenye kambi moja katika kijiji cha Garuwa huko Bali.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.