Sherehe ya kwanza kihistoria kufanyika Burundi kuitambulisha katiba mpya

Hata hivyo wapinzani na baadhi ya nchi za kigeni wamekosoa mchakato huo mzima kwamba haukuzingatia sheria

Sherehe ya kwanza kihistoria kufanyika Burundi kuitambulisha katiba mpya

Hata hivyo wapinzani na baadhi ya nchi za kigeni wamekosoa mchakato huo mzima kwamba haukuzingatia sheria

05 June 2018 Tuesday 16:03
Sherehe ya kwanza kihistoria kufanyika Burundi kuitambulisha katiba mpya

NCHI ya Burundi inatarajia kuitambulisha katiba yake mpya kesho kutwa katika shughuli itakayofanyika katika mkoa wa Gitega.

Kwa mujibu wa BBC eneo hilo ndiko kuliko zinduliwa rasmi mchakato wa katiba, lakini pia kampeni ya chama madarakani CN DD/FDD ya kuipiga debe katiba hiyo.

Hata hivyo wapinzani na baadhi ya nchi za kigeni wamekosoa mchakato huo mzima kwamba haukuzingatia sheria na katiba mpya inanuwia kumbakiza madarakani Rais Pierre Nkurunziza hadi mwaka 2034.

Taarifa ya Ikulu ya Burundi imetoa mwaliko kwa magavana wote na Wakuu wa tarafa za Burundi kushiriki kwenye sherehe hizo.

Wamealikwa pia wawakilishi wa vyama vya kisiasa, asasi za kiraia pamoja na Viongozi wa kidini.

Itakuwa mara ya kwanza katika historia ya Burundi kuwa na sherehe za kuipokea katiba mpya.

Wadadisi wa siasa za Burundi wanahisi utaratibu huo mpya ni ujumbe wa Rais Nkurunziza kwamba zama yake ya kukamilisha shughuli ya katiba ambayo yeye ameipigia debe kwamba inakuja kuipa Burundi hadhi na Uhuru wake kamili wa kujitawala.

Lakini pia ni ujumbe ambao kiongozi huyo anaupeleka kwa Jumuiya ya kimataifa hususani, mataifa ambayo yalitilia shaka na kukosoa mpango mzima wa marekebisho ya katiba wakitaja kwamba uliandaliwa kinyume cha sheria.

Ni hivi karibuni tu Umoja wa mataifa, na baadhi ya nchi za magharibi washirika wa zamani wa Burundi kama Ufaransa na Ubelgiji walikemea vikali mchakato mzima wa katiba kwamba uligubikwa na dosari nyingi na kwamba katiba hiyo mpya inatishia hata maridhiano ya kitaifa na uwakilishi wa makabila kwa Mujibu wa Mkataba wa Aman iwa Arusha.

Madai ambayo yamepingwa vikali na Wakuu wa Burundi.

Katiba hii mpya ambayo inaanza kutekelezwa siku ya Alhamis itageuza mambo mengi kwenye taasisi za maongozi ya taifa, lakini pia kutoa fursa kwa Rais Pierre Nkurunziza kuweza kuwania uongozi wa nchi hadi mwaka wa 2034.

Katiba pia inaanza kutekelezwa wakati mazungumzo ya amani yakiwa yamekwama baada ya serikali kukata kuketi meza moja na wapinzani.

BBC

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.