Temeke hakuna michepuko tena, kamanda wa usalama barabarani asema

Temeke hakuna michepuko tena, kamanda wa usalama barabarani asema

08 June 2018 Friday 10:59
Temeke hakuna michepuko tena, kamanda wa usalama barabarani asema

Na Mwandishi Wetu

SUALA la baadhi ya madereva wilayani Temeke, Mkoani Dar es Salaam kupita njia za michepuko wakati wa foleni kubwa halipo kwa sasa kwa sababu mbali mbali, jeshi la Polisi la mkoa huo limesema.

Akizungumza na Azania Post leo Ijumaa, Kamanda wa Usalama barabarani mkoa wa Temeke, SSP Victor Ayo amesema madereva wengi hawatanui kwenye barabara kwani suala hilo limedhibitiwa.

Amesema kuwa mbali ya kudhibitiwa kupita njia za michepuko, miundombinu mingi ya barabara wilayani humo hairuhusu kufanya hivyo.

Hata hivyo amebainisha changamoto kadhaa za kiusalama wa magari na waenda kwa miguu katika baadhi ya maeneo.

Kwa mujibu wa kamanda huyo moja ya changamoto ni ukosefu wa stendi ya daladala katika eneo la Tandika ambapo imekuwa bughudha kwa wenye magari na waenda kwa miguu.

Alisema kuwa kutokuwepo kwa stendi, kunapelekea daladala hizo kushusha na kupakia abira kwenye mitaa.

Aliongeza kuwa maeneo ya Mbagala, Mbande na Kisewe kuna shida ya miundombinu hasa ubovu wa barabara.

Kuhusu foleni alisema kuwa mara nyingi inakuwepo wakati wa asubuhi na jioni ambapo wamekuwa wakijitahidi sana kukabiliana nalo.

Katika kukabiliana alisema kuwa wanabuni njia mbili kuanzia enep la Misheni hadi Uhasibu wakati wa asubuhi, na imekuwa ikisaidia sana kuvuta magari mengi kuwahi.

Alisema kwa mujibu wa sheria ya usalama barabarani 73(4) jeshi la Polisi linaruhusiwa kutafuta njia mbadala kunapokuwa na tatizo la foleni.

Aliwataka madereva wa bodaboda kutii sheria bila shuruti hasa pale wanaposimamishwa kwa ajili ya ukaguzi badala ya kukimbia kunakosabisha ajali.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.