banner68
banner58

Trump , Kim sasa mambo damu damu, kuanza kutembeleana rasmi

Wachanganuzi wanasema kuwa ni nafasi nzuri ya kuendeleza uhusiano baina ya nchi mbili, lakini wakosoaji wanasema kuwa hii huenda ikasababisha majaribio ya...

Trump , Kim sasa mambo damu damu, kuanza kutembeleana rasmi

Wachanganuzi wanasema kuwa ni nafasi nzuri ya kuendeleza uhusiano baina ya nchi mbili, lakini wakosoaji wanasema kuwa hii huenda ikasababisha majaribio ya...

13 June 2018 Wednesday 09:39
Trump , Kim sasa mambo damu damu, kuanza kutembeleana rasmi

Na Mwandishi Wetu

KIONGOZI wa Korea Kaskazini Kim Jong Un na Rais wa Marekani Donald Trump wamekubaliana kutembeleana katika nchi zao hapo baadaye.

Taarifa zinasema kuwa Kim amekubali kuitembelea Marekani, naye Trump ataitembelea Korea Kaskazini wakati wowote.

Inasemekana kuwa viongozi hao walipeana mialiko hiyo wakati wa mkutano wa historia baina ya wawili hao nchini Singapore Jumanne.

"Viongozi ao wawili wakuu walikubali mwaliko wa kila mmoja," shirika la KCNA limeripoti.

Kenye tamko lake la kwanza kabisa tangu kutokea kwa mkutano huo, Bw Kim amenukuliwa akisema kwamba kuna haja ya "dharura" ya kusitisha "hatua za kijeshi za uchokozi zinazokera kati ya mataifa" hayo mawili.

Alisema nchi zote mbili zinafaa "kujitolea kujizuia kufanya uchokozi" na "kuchukua hatua za kisheria na kitaasisi kuhakikisha hilo linafanyika", KCNA wameripoti.

Wachanganuzi wanasema kuwa ni nafasi nzuri ya kuendeleza uhusiano baina ya nchi mbili, lakini wakosoaji wanasema kuwa hii huenda ikasababisha majaribio ya mapinduzi ya serikali Korea kaskazini.

Hakuna tarehe iliyotolewa kwa ziara hiyo lakini katika mahojiano na shirika la habari la Fox News, Trump alikuwa amesema baadaye kwamba Kim anakaribishwa kuzuru White House wakati wowote ule utakaofaa.

Hayo yakijiri, Marekani imewahakikishia washirika wake katika eneo la Asia Mashariki kwamba itatekeleza majukumu yake ya kuwalinda.

Hii ni baada ya Rais Trump kukubali kufutilia mbali mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini baada ya kukutana na Bw Kim.

Korea Kaskazini imekuwa ikiitaka Marekani kusitisha mazoezi hayo yanayofanyika kila mwaka kwa muda mrefu.

Uhasama kati ya Marekani na Korea Kaskazini ulikuwa ukizidi kila mazoezi hayo yanapoanza.

Hatua ya Trump kukubali kusitisha mazoezi hayo ilionekana kama 'kubadilisha msimamo pakubwa' kwa Marekani na iliwashangaza washirika wa Marekani katika kanda hiyo.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.