Trump kukutana na hasimu wake kesho chini ya ulinzi wa kihistoria

Baada ya safari ya saa 20 Rais huyo wa Marekani aliwasili nchini humo akitokea Canada alikohudhuria mkutano wa kundi la mataifa yaliyostawi kiviwanda la G7 huku

Trump kukutana na hasimu wake kesho chini ya ulinzi wa kihistoria

Baada ya safari ya saa 20 Rais huyo wa Marekani aliwasili nchini humo akitokea Canada alikohudhuria mkutano wa kundi la mataifa yaliyostawi kiviwanda la G7 huku

11 June 2018 Monday 09:04
Trump kukutana na hasimu wake kesho chini ya ulinzi wa kihistoria

Na Mwandishi Wetu

MAANDALIZI ya mkutano baina ya Rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un yamekabilika mara baada ya wote wawili kuwasili huko Singapore, huku ulinzi mkali ukiendelea kuimarishwa.

Trump amewasili Singapore jana Jumapili kuhudhuria mkutano wa kihistoria na kiongozi wa Korea Kaskazini kuhusu matumizi ya silaha za nyuklia.

Trump aliwasili katika uwanja wa ndege wa jeshi la Singapore wa Paya Lebar akiwa katika ndege yake ya Air Force One, akitarajia kuweka msingi wa mkataba wa nyuklia na mojawapo ya mahasimu wabaya kabisa wa Marekani.

Baada ya safari ya saa 20 Rais huyo wa Marekani aliwasili nchini humo akitokea Canada alikohudhuria mkutano wa kundi la mataifa yaliyostawi kiviwanda la G7 huku akilakiwa katika uwanja wa ndege wa kijeshi na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Singapore Vivian Balakrishnan.

Aliwasili saa chache baada ya Kim kutua Singapore katika ziara yake ndefu ya kigeni kama mkuu wa nchi. Viongozi hao wawili wanatarajiwa kukutana siku ya Jumanne (12.06.2018) katika kisiwa cha mapumziko cha Sentosa kwa mkutano wa kilele unaowekewa matumaini makubwa; mazungumzo ya kwanza kati ya rais wa Marekani aliye madarakani na kiongozi wa Korea Kaskazini.

Miezi michache iliyopita mkutano kama huyo haungefikirika wakati Trump na Kim walipokuwa wakitupiana maneno ya matusi na vitisho vilivyoongeza hofu ya kutokea vita katika rasi ya Korea. Lakini mfululizo wa jitihada za kidiplomasia zilizoihusisha Korea Kaskazini, Korea Kusini na Marekani, zilipunguza hali ya wasiwasi na kumfanya Trump mwezi Machi kwa haraka kuukubali mualiko wa Kim kukutana naye.

Azania Post

Updated: 11.06.2018 09:15
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.