Uganda kujenga 'Makumbusho ya Iddi Amin' ili kuvutia watalii

Iddi Amin atakumbukwa kwa unyama wa kutisha aliofanya dhidi ya watu wake miaka ya 1970

Uganda kujenga 'Makumbusho ya Iddi Amin' ili kuvutia watalii

Iddi Amin atakumbukwa kwa unyama wa kutisha aliofanya dhidi ya watu wake miaka ya 1970

01 June 2018 Friday 19:56
Uganda kujenga 'Makumbusho ya Iddi Amin' ili kuvutia watalii

Uganda inatarajia kuvutia watalii kwa kutumia makumbusho ya vita kuonyesha zama za giza kabisa katika historia yake.

Unyama uliofanywa chini ya utawala Rais wa zamani Idi Amin wa miaka minane na jeshi la Lord’s Resistance Army (LRA) unatakiwa kuwekwa kwenye kumbukumbu.

"Tunataka kuweka mambo wazi," Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Utalii wa Uganda Stephen Asiimwe aliiambia BBC.

Makumbusho ya vita ya Uganda, ambayo bado haijajengwa, itaonyesha pia historia ya awali kabla ya ukoloni na wakati wa ukoloni nchini humo.

"Historia inapata utajiri zaidi, ni kama divai nyekundu - inapendeza zaidi kama miaka inavyozidi kwenda mbele," Mr Asiimwe alisema.

Alikiambia kipindi cha Newsday cha BBC kuwa mradi huo haujakusudiwa kuhadhibu hisia za watu.

"Niliishi katika zama za Iddi Amin kama kijana mdogo, wazazi wa wanafunzi wenzangu waliuawa na serikali," alisema.

"Hata hivyo huwezi kuikimbia historia. Huo ndiyo ukweli."


Idi Amin:

  • Alijiunga na jeshi la kikoloni – the King’s African Rifles – akiwa na miaka 20
  • Ulichukua madaraka ya kuiongoza Uganda mwaka wa 1971, karibu miaka 10 baada ya uhuru wa Uganda
  • Watu 400,000 wanaaminika kuwa waliuawa chini ya utawala wake
  • Alifukuza watu wote wenye asili ya Asia nchini Uganda mwaka wa 1972, wakiwashtakiwa kuwa wahujumu uchumi
  • Alibadili dini na kuwa muislamu, akachukua wake watano, akazaa watoto kadhaa na akasisitiza kuitwa "Big Daddy"
  • Alijitangaza mwenyewe kuwa Mfalme wa Scotland, akapiga marufuku na sketi fupi na zinazobana, na alijizawadia Victoria Cross
  • Aliondolewa madarakani na askari wa Tanzania na wapiganaji waliokuwa wanaishi uhamishoni wa Uganda mwaka wa 1979
  • Alifariki nchini Saudi Arabia mwaka 2003

Asiimwe alisema kwamba kila sehemu ina utamaduni na vivutio vyake.

"Nchini Uganda tunawanyama pori, lakini tunajaribu kutazama historia yetu ya nyuma."

Kuonyesha historia ya Uganda kutalifanya taifa hilo la Afrika Mashariki kuwa sehemu nzuri kwa ajili ya watalii kutembelea, aliongeza.

Hivi karibuni, Waganda wamelazimika kukabiliana na kundi la LRA, ambalo limekuwa linapambana kutaka kusimika serikali inayofuata misingi ya amri kumi za Mungu za kwenye Biblia.

Kundi hilo liliundwa nchini Uganda zaidi ya miongo miwili iliyopita, na limekuwa maarufu kwa kukata miguu ya watu na kuteka watoto kwa ajili ya kuwatumia kama askari na watumwa wa ngono.

Kiongozi wake, Joseph Kony, anatakiwa kwa uhalifu wa kivita na kundi hilo linaendelea kufanya kazi kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Jamhuri ya Afrika Kati.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.