Uganda kutoza kodi watumiaji wa Whatsapp na Facebook ‘kuzuia umbea’

Rais Yoweri Museveni alishinikiza mabadiliko hayo, akisema kuwa mitandao ya kijamii inachochea umbea

Uganda kutoza kodi watumiaji wa Whatsapp na Facebook ‘kuzuia umbea’

Rais Yoweri Museveni alishinikiza mabadiliko hayo, akisema kuwa mitandao ya kijamii inachochea umbea

31 May 2018 Thursday 20:28
Uganda kutoza kodi watumiaji wa Whatsapp na Facebook ‘kuzuia umbea’

Bunge la Uganda limepitisha sheria iliyojaa utata ya kutoza kodi kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii.

Inatoza shilingi 200 [$ 0.05, £ 0.04] ambayo ni sawa na shilingi 130 ya Kitanzania, kila siku kwa ushuru wa watu kwa kutumia majukwaa ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia mitandao kama Facebook, Whatsapp, Viber, na Twitter.

Rais Yoweri Museveni alishinikiza mabadiliko hayo, akisema kuwa mitandao ya kijamii inachochea umbea.

Sheria inapaswa kuanza kazi tarehe 1 Julai lakini kuna mashaka juu ya jinsi itakavyotekelezwa.

Sheria mpya ya kodi pia itaweka kodi nyingine mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kodi ya 1% ya thamani ya jumla ya shughuli za kifedha kupitia simu - ambazo makundi ya kiraia yanalalamika kuwa yataathiri maskini wa Uganda ambao hawatumii huduma za kibenki.

Waziri wa Fedha David Bahati aliliambia bunge la Uganda kwamba ongezeko la ushuru lilihitajika ili kusaidia Uganda kulipa deni lake la kitaifa.

Wataalam na angalau mtoa huduma mkubwa mmoja wa huduma ya mtandao wameonyesha wasiwasi wao juu ya jinsi kodi za kila siku kwenye mitandao ya kijamii itakavyotekelezwa, mwandishi wa BBC Catherine Byaruhanga anaripoti kutoka Uganda.

Serikali inajitahidi kuhakikisha kwamba kadi zote za SIM za mkononi zinaandikishwa kwa usahihi.

Na kati ya wamiliki wa simu milioni 23.6 nchini humo, milioni 17 tu hutumia mtandao wa internet, shirika la habari la Reuters kinaripoti.

Kwa hiyo haijulikani jinsi mamlaka nchini humo zitaweza watu ambao wanaingia katika mitandao ya kijamii.

Mr Museveni alishinikiza uwepo wa sheria ya mitandao ya kijamii tangu mwezi Machi. Alimwandikia barua Waziri wa Fedha Matia Kasaija akisisitiza kwamba mapato yatakayokusanywa kutokana na mitandao ya kijamii yatasaidia nchi "kukabiliana na matokeo ya umbea (olugambo)".

Lakini alisema kuwa haipaswi kuwepo na kodi kwenye matumizi ya kawaida ya mtandao kwa kuwa una manufaa kwa "elimu, utafiti au kutafuta taarifa".

Wakosoaji wakati huo walisema sheria hiyo ingepunguza uhuru wa kujieleza.

Kasaija alikataa madai hayo kuwa sheria mpya inaweza kupunguza matumizi ya mtandao nchini humo.

"Tunatafuta fedha ili kudumisha usalama wa nchi na kupanua umeme ili watu waweze kufurahia zaidi mitandao ya kijamii, mara nyingi, mara nyingi zaidi," aliiambia Reuters mwezi Machi.

Mitandao ya kijamii imekuwa chombo muhimu cha kisiasa nchini Uganda kwa chama tawala na upinzani, mwandishi wetu anasema.

Upatikanaji wa mitandao ya kijamii ulifungwa wakati wa uchaguzi wa rais mwaka 2016. Rais Museveni alisisitiza wakati huo kwamba hatua hiyo ilifanyika ili "kuacha kueneza uongo".

Nchi nyingine za Mashariki mwa Afrika zimekuwa zikipitisha sheria ambazo zinakosolewa na wanaharakati kuwa zinaathiri uhuru wa kujieleza.

Serikali ya Tanzania ilishinda kesi mahakamani mnamo tarehe 29 Mei dhidi ya wapinzani wa sheria mpya ambayo inawataka wanablogu kulipa ada ya leseni na kuweka wazi wafadhili wao wa kifedha.

Nchini Kenya, sheria mpya ya uhalifu wa kimtandao yaani cybercrime law ambayo ilianza kutumika Mei 30 mwaka huu.

Waandishi wa habari na wanablogu kupitia mahakama walifanikiwa kuzuia sheria ya Kenya kupiga marufuku habari "ya uwongo" ambayo wanasema ni jaribio la kuingilia uhuru wa vyombo vya habari vya kujitegemea.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.