Uwepo wa benki moja waleta changamoto kubwa sana, asema waziri wa afya

Uwepo wa benki moja waleta changamoto kubwa sana, asema waziri wa afya

15 June 2018 Friday 12:41
Uwepo wa benki moja waleta changamoto kubwa sana, asema waziri wa afya

Na Mwandishi Wetu

HUDUMA za utoaji damu nchini Sudan ya Kusini zinakabiliwa na changamoto nyingi kutokana na kuwepo kwa benki moja tu kwa ajili ya kazi hiyo, waziri wa Afya amesema.

Akizungumza waziri huyo Bw Riek Gai Kok amesema Sudan Kusini imekumbwa na hali mbaya ya miundombinu ya afya, inayokwamisha huduma za utoaji damu nchini kote, lakini juhudi zimefanywa kwa ajili ya kuboresha hali hiyo.

Amesema kwa sasa kuna benki moja tu ya damu nchini Sudan Kusini, hali ambayo imesababisha vifo vya watu wengi kutokana na ukosefu wa damu. Ametoa wito kwa washirika wa maendeleo kutoa  misaada ili kuhimiza huduma za utoaji damu nchini humo.

Jana serikali hiyo imeadhimisha siku ya kuchangia damu duniani ikitoa wito wa kuongeza uwekezaji kwenye sekta  hiyo nyeti nchini humo.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.