Video: Juliana Raymond akitoa ushuhuda wa faida za biashara za mtandaoni

Mtu anaweza kutengeneza kipato kizuri tu kwa biashara za mtandaoni

Video: Juliana Raymond akitoa ushuhuda wa faida za biashara za mtandaoni

Mtu anaweza kutengeneza kipato kizuri tu kwa biashara za mtandaoni

02 June 2018 Saturday 16:13
Video: Juliana Raymond akitoa ushuhuda wa faida za biashara za mtandaoni

Na Amini Nyaungo

Kutokana na kubadilika kwa Sayansi na Teknolojia, dunia imekuwa kama kijiji kwani kila kitu ambacho mtu anaweza kuwa anahitaji, anakipata wakati huo huo, hata kama kipo nje ya mipaka ya nchi.

Watu wengi, hususan vijana wameweka makazi mitandaoni, hususan katika mitandao ya kijamii.

Na huko hasa ndipo mtu huweza kufanya mambo mbalimbali ya kimaisha kama biashara na mengineyo.

Lakini pia, wengine kuwafurahisha kwa kuonesha picha zao na vitu vingine vya burudani.

Biashara nyingi kwa sasa zimehamia mtandaoni `online` na wafanyabiashara huitumia mitandao ya kijamii kujinufaisha kimapato.

Juliana Raymond, msomi wa shahada ya Elimu pale Chuo Kikuu cha Dar es salaam, alianza kwa kuuza maandazi mtandaoni na wafanyakazi wenzake ili kujikimu kwa kipato na sasa amefika mbali.

Mwandishi wa Azania Post Amini Nyaungo amefanya mahojiano na Juliana Raymond ambaye ametoka kuuza maandazi hadi kumiliki gari na kusaidia familia yake kupitia biashara ya mtandaoni.

Juliana kupitia kampuni yake ya Thanks Much ametumia vizuri biashara ya hiyo hadi kufikia kununua gari kwa ajili ya kuwafuata wateja wake popote walipo hapa Dar es Salaam, pia kuwasaidia wadogo zake na familia nzima.

Biashara yake imekuwa hadi kusambaza karibuni mikoa yote Tanzania Bara.

Swali: Mambo vipi unaitwa nani?

Jibu: Naitwa Juliana Raymond jina la biashara mtandaoni naitwa Thanks Much.

Swali: Biashara zako zilianzaje kupitia Online?

Jibu: Takribani miaka minne nimeanza kuuza maandazi, chapati na bagia ambapo niliwauzia wateja wangu ambao nilikuwa nafanya nao kazi. Kwa sasa nashukuru Mungu hapa nilipofikia.

Swali: Biashara ya maandazi ulikuwa unapata kiasi gani kwa siku?

Jibu: Nilikuwa nauza maandazi mia mbili kwa siku ambapo kwa mwezi nimepata ilikuwa kama laki sita ambapo ukitoa na gharama nyingine ilikuwa inapatikana kama lakini tatu faida.

Swali: Kiwango chako cha Elimu kimefikia wapi?

Jibu: Nimemaliza Mlimani (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) `Bachelor` ya Elimu na utamaduni

Swali: Unawaambiaje wanaoona noma kuuza maandazi wakati wakiwa na Elimu kama yako?

Jibu: Mwanamke unapaswa kujitambua, hiki ni kipindi cha kuanza kujisaidia mwenyewe, usisubiri taasisi, au familia ikusaidie.

Swali: Baada ya kuuza maandazi umehamia biashara gani?

Jibu: Haikuwa rahisi baada ya kutoka katika biasharaya maandazi. Nimehamia katika mavazi, pia nimeongeza hadi ufugaji wa kuku na lishe kwa pamoja.

Swali: Umeingiaje Online hadi kusambaa Tanzania nzima?

Jibu: Nimekaa na kufikiria nikagundua mitandao ya kijamii inaweza kukutoa kutoka ulipo hadi sehemu nyingine, nikawa natumia group zangu za WhatsApp kwa marafiki zangu, pia nikaona dhahiri mitandao ya kijamii kama vile, Facebook WhatsApp na Instagram ni sehemu nzuri sana ya kupata soko.

Swali: Uliwavutaje wateja?

Jibu: Nimeanza na followers 24, ila nimegundua ukitumia picha nzuri pamoja na video yasiwe maelezo mengi utakuwa umewavuta `followers` ku-like ukurasa wako na hao ndio watakusaidia katika biashara zako. Kwa sasa nina followers 18K

Mteja anapenda content ya video kuliko maelezo yaliyo marefu, biashara yangu ikafika hadi kuniita Juli Mmachinga, ambapo lengo lao lilikuwa wanikatishe tamaa, maana kweli nilikuwa nauza kila kitu kasoro nyumba.

Swali: Una changamoto gani katika biashara yako?

Jibu: Ni kweli zipo kuna mteja aliwahi kutuma pesa katika namba yangu kisha anapiga katika mtandao husika anataka pesa irudishwe yaani `Reversal` au anaweza akadanganya amekosea kutuma pesa, mwingine anasema hakutaka kutuma kiasi hicho.

Ili kudhibiti wizi huo nimejipanga sana natumia True caller na caller records ili kupata mawasiliano yake endapo atapiga katika mtandao husika nipate sauti yake na uthibitisha kamili.

Katika video inayofuata utapata kuona namna alivyofanikiwa hadi kununua gari kwa ajiri ya biashara yake. Lakini pia ameajiri watu wanne katika kampuni yake ya Thanx Much.

Pia utapata kujua namna gani ukitaka kuanza biashara hii ya mtandaoni kitu gani ufanye.

Azania Post

Updated: 02.06.2018 16:28
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.