Vikongwe wawili wafungwa jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka 10

Vikongwe wawili wafungwa jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka 10

06 June 2018 Wednesday 17:36
Vikongwe wawili wafungwa jela maisha kwa kumbaka mtoto wa miaka 10

Na Mwandishi Wetu

MAHAKAMA kuu nchini Kenya imewahukumu jela kifungo cha maisha vikongwe wawili wenye umri wa miaka zaidi ya themanini baada ya kuwakuta na hatia ya kumlawiti kijana wa kike mwenye umri wa miaka kumi.

Vikongwe hao waliohukumiwa ni Tom Mungai (83) na Mureithi Ngari (88) inadawa kuwa walitenda vitendo hivyo katika kijiji cha Tangi Tano Kaunti ya Nakuru.

Ilidaiwa kuwa Mungai alifanya kitendo hicho tarehe 16 Novemba mwaka huo na Ngari alifanya awali tarehe 14 Novemba 2015.

Mtoto huyo alidai kuwa alikutana na Mungai Novemba mwaka 2015 na alimshawishi kwenda nyumbani kwake na kumpatia nyama.

Anasema kuwa aliongozana na mzee huyo alimpatia ugali na nyama siku ya kwanza na baadaye akamruhusu kurudi kwao.

Aliongeza kuwa siku nyingine tena alimuani mzee huyo na kwenda kwake  na kumpatia karoti kula baadaye kumueleza apande kitandani na kumfanyia matendo hayo mabaya.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.