Waabudu shetani wajitokeza hadharani nchini Marekani

Wazindua sanamu ya Mungu ‘Baphomet’ kwenye ofisi ya serikali ya Jimbo la Arkansas

Waabudu shetani wajitokeza hadharani nchini Marekani

Wazindua sanamu ya Mungu ‘Baphomet’ kwenye ofisi ya serikali ya Jimbo la Arkansas

20 August 2018 Monday 16:46
Waabudu shetani wajitokeza hadharani nchini Marekani

Waumini wa shetani wamesherehekea kuzinduliwa kwa sanamu la kiumbe mwenye kichwa cha mbuzi akiwa na mabawa nje ya jingo la serikali nchini Marekani.

Waumini wa hekalu la kishetani walipeleka sanamu hilo lenye urefu wa futi nane na nusu, karibu na jingo la makao makuu ya serikali ya jimbo la Arkansas katika jiji la Little Rock jana.

Sanamu hilo la kutisha lenye mabawa linaonekana likiwa limekaa kwenye kiti cha enzi likiwa na alama ya pentagram.

Maandamano yalitokea baada ya bunge la jimbo la Arkansas kukubali ombi la kuweka amri kumi za Mungu kwenye jengo la serikali.


Pembeni yake anaonekana mtoto mdogo akitazama sanamu hiyo ya mtu huyo mwenye kichwa cha mbuzi kwa macho ya mahaba.

Sanamu hiyo ilikuwa ni sehemu ya maandamano nje ya jingo la serikali katika eneo ambalo kumbukumbu ya Amri Kumi za Mungu (katika biblia) imewekwa kupinga kufuru hiyo.

Sanamu hiyo tayari imeondolewa katika eneo hilo lakini Hekalu la Kisherani limefungua kesi mahakamani kutaka sanamu hilo kurejeshwa ili kudhihirisha uhuru wa kuabudu ambao upo kwenye katiba ya Marekani.

Sanamu hiyo ilisababisha maandamano kutoka kwa wanaharakati wa Kikristo.

Kanisa la Kishetani, ambalo lina wafuasi ulimwenguni kote ambao hudai uhuru wa kuabudu, linadai kwamba liliwaandikia wabunge wa jimbo hilo kutaka sanamu hilo la Baphomet kuruhusiwa.

Akizungumza katika maandamano hayo Lucien Greaves, msemaji na mwanzilishi wa Hekalu la Kishetani alisema: “Tukio hili linatazamiwa kuwa kusanyiko ambalo Hekalu la Kishetani litakuwa likisheherekea uhuru wa kuabudu pamoja na wasemaji wa Kikristo na wale wasiokuwa na dini.

Jiwe lenye amri 10 za kwenye biblia nje ya jengo la Bunge la Jimbo la Arkansas nchini Marekani ambalo lilisababisha maandamano miongoni wa waabudu shetani


“Watu wa Imani nyingi wataungana pamoja huko kwenye Capitol (jengo la bunge) kupinga jitihada za Bunge la Jimbo la Arkansas kupendelea dini moja dhidi ya dini nyingine.”

Jiwe lenye Amri Kumi za Mungu liliwekwa nje ya jengo la serikali mwaka jana baada ya muswada ambao uliungwa mkono na seneta wa chama cha Republican Jason Rapert kupitishwa, kulingana na gazeti la Independent.

Rapert alitoa tamko kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook akisema: “Haijalishi kile hawa wenye msimamo mkali wanaweza kudai, itakuwa siku yenye baridi sana huko kuzimu kabla ya sanamu inayotuchukiza itasimamishwa moja kwa moja katika viwanja vya jingo la Arkansas State Capitol.

“Haki zetu kujenga kielelezo chetu ilidhihirishwa kupitia mifumo ya uchaguzi na kibunge na imethibitishwa na mfumo wa kimahakama.

“Hakuna kilicho kizuri Zaidi ya uhuru wa wachache, ambao haki yao ya kisheria na kisiasa ni njia tu ya kuwafurahisha wasio na akili na kuwastarehesha wenye kiburi.

“Utaratibu uliowekwa ulifuatwa na mikutano ya uwazi na ile ya hadhara kupata maoni juu ya kuwekwa kwa jiwe la Amri Kumi za Mungu.”

Ukweli juu ya Waabudu Shetani

  • Mahekalu ya Kishetani hujiona kama ‘kundi la kidini’ ambalo pia lina waharakati na waumini wa kisiasa ambayo yanafanya kazi kupigania usawa, haki ya kijamii, na kutenganishwa kwa kanisa na taifa.
  • Kundi hilo husema kwamba hawamuamini Shetani lakini hutumia neon kuwakilisha “mwasi wa milele” ambaye yupo nje ya mamlaka na sheria za kijamii na anasimamia busara na haki.
  • Kundi hilo lina wafuasi ulimwenguni kote – kundi kubwa Zaidi lipo huko Detroit, Michigan nchini Marekani.
  • Mei 2014 ibada nyeusi ilifanywa katika Chuo Kikuu cha Havard japokuwa ililazimika kuhamishiwa nje ya chuo kutokana na upinzani wa kanisa katoliki.
  • Kundi hilo limekuwa likipinga vikali marufuku dhidi ya utoaji mimba, likiwakaribisha wakimbizi na hata kuwa program baada ya masaa ya kawaida ya shule katika mashule.
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.