Wafungwa wateka gereza, watoa masharti

Wafungwa wateka gereza, watoa masharti

08 October 2018 Monday 13:22
Wafungwa wateka gereza, watoa masharti

KATIKA hali isiyo ya kawaida, wafungwa wanaoshikiliwa kwenye gereza la Juba nchini Sudan Kusini wanadaiwa kuliteka gereza hilo huku wakiwa na silaha ikiwemo bunduki na visu, wakishinikiza kuachiliwa huru kwa wafungwa wa kisiasa.

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Swahili, umeripoti kwamba wafungwa hao ambao idadi yao rasmi haijajulikana, walimzidi nguvu mlinzi wa lango la kuingilia la gereza walilokuwamo kisha kuvunja milango kwa risasi, na kufanikiwa kuchukua bunduki na visu kutoka ndani ya ghala la kuhifadhia silaha.

Wafungwa hao wanadaiwa kuchukua hatua hiyo ikiwa ni sehemu ya shinikizo kwa Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir la kumtaka kutekeleza ahadi yake ya kuwaacha huru wafungwa wa kisiasa. Na kwamba mamlaka nchini humo inaendelea na mazungumzo dhidi ya wafungwa hao waliojihami kwa silaha.

Jeshi la Polisi nchini humo limekanusha madai hiyo, likieleza kuwa wafungwa takribani 60 kati ya 400 walioko kwenye gereza hilo, ndiyo walioanzisha vurugu hizo na mgomo.

Updated: 15.05.2019 10:39
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.