banner68

Waziri Jafo atangaza ajira 6,180 watumishi afya

Waziri Jafo atangaza ajira 6,180 watumishi afya

10 July 2018 Tuesday 15:39
Waziri Jafo atangaza ajira 6,180 watumishi afya

Serikali imetangaza ajira mpya za watumishi 6,180 wa kada mbalimbali za afya katika Mamlaka za serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jaffo amesema ajira hizo ni utekelezaji Ilani ya chama cha mapinduzi pamoja na ahadi ya Serikali katika kuboresha huduma za afya nchini.

Aidha, waombaji wote waliochaguliwa katika ajira hizo wametakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi ndani ya siku 14 kuanzia sasa na atakayeshindwa nafasi yake itachukuliwa na mtu mwingine.

Jafo amesema ajira hizo zimetokana na kibali kilichoandikwa kwa serikali cha kuajiri watumishi wa kada mbalibali wa sekta ya afya nchini.

Amesema kuwa kibali hicho ni mwendelezo wa kibali cha ajira kwa kada za afya 3,152 kilichotolewa mwezi Juli 2017 kwa lengo la kukabiliana na changamoto za utumishi katika vituo vya afya nchini.

Dar24

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.