Ziwa Rukwa sasa kufanyiwa utafiti mkubwa ili linufaishe wananchi

Ziwa Rukwa sasa kufanyiwa utafiti mkubwa ili linufaishe wananchi

30 May 2018 Wednesday 15:59
Ziwa Rukwa sasa kufanyiwa utafiti mkubwa ili linufaishe wananchi

Na Mwandishi Wetu

TAASISI ya Utafiti wa samaki itapewa fedha kwa ajili ya kuangalia mazao yaliyopo Ziwa Rukwa kama yatanufaisha wananchi, Bunge limeambiwa.

Hayo yamebainishwa na Naibu waziri wa Uvuvi na Umwagiliaji, Abdallah Ulega alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Songwe, Philip Mulugo (CCM) aliyetaka kujua mikakati ya serikali katika kuhakikisha ziwa hilo linanufaisha wanachi kwa kuliwekea mazingira ya kuwa na samaki wengi.

Alisema kuwa wakati mwingine ziwa hilo linafungwa kwa shughuli za uvuvi ili kufanya samaki wakue, lakini hali inakuwa vilevile na kuitaka serikali kutoa tamko.

Naibu Waziri Ulega alisema kuwa serikali imetenge kiasi cha fedha kwa taasisi ya Tafiri na kuielekez kuangalia hatima ya ziwa Rukwa ili liweze kuwanufaish wanachi.

Alisema kuwa fedha hizo zitatmika kufanya mambo mbali mbali ikiwemo kuangalia kiasi na aina ya samaki wanaofaa kuvuliwa.

Mwishoni mwa mwaka jana iliripotiwa kuwa uongozi wa mkoa wa Rukwa ulisimamisha shughuli za uvivi katika ziwa hilo.

Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alikaririwa akisema kuwa amesimamisha shughuli za uvuvi katika ziwa Rukwa hadi hapo wataalamu wa afya watakapojiridhisha kuwa hakuna ugonjwa wa kipindupindu katika kambi za uvuvi zinazozunguka ziwa hilo na Mkoa kwa jumla.

Alisema kuwa athari inayopatikana katika kambi hizo za uvuvi zitawaathiri wala samaki unaotokana na uvuvi wa ziwa hilowaliopo na kuongeza kuwa wale wote wanaovua samaki waliopiga kambi katikakati ya ziwa waache kuvua mara moja na wasiruhusiwe kuingia katika ili kuweza kuudhibiti ugonjwa huo.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.