Aliyejifanya mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia, afungwa jela

Aliyejifanya mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia, afungwa jela

05 June 2019 Wednesday 12:29
Aliyejifanya mwana wa Mfalme wa Saudi Arabia, afungwa jela

Anthony Gignac ambaye kwa muda mrefu ameishi kwa kutumia jina la Mwana Mfalme wa Saudi Arabia  Prince Khalid Al Saudi amekuhumiwa kifungo cha miaka 18 jela kwa kosa hilo.

Gignac aliweza kuishi maisha ya anasa licha ya kukamatwa sehemu mbali mbali kwa kujiita Prince Khalid bila kujua kuwa Prince Khalid mwenyewe ni mtu mzima mwenye umri wa miaka 79 ambaye muda mwingi anaishi jiji la Mecca nchini Saudi Arabia eneo ambalo alikuwa mtawala kwa muda mrefu

Gignac  mwenye asili ya mataifa ya Marekani na Columbia na mwenye umri  nusu ya Prince Khalid Al Saud Mwenyewe.
Ni Tapeli wa kimataifa aliyeweza kuwatapeli   watu kwa kuwauzia  bidhaa bandia  nchini Marekani hadi 2017 alipokamatwa na kushtakiwa kwa kuuza bidhaa  feki kwa nia ya kuwadanganya wawekezaji zenye thamani ya  dola za kimarekani milion 8.

Imeripotiwa  aliweza kubadili picha kwenye mitandao ya kompyuta aliyokuwa anaumiliki kwa kuweka picha mbalimbali za wana ukoo wa Mfalme  wa Saudi  Arabia ili kuwadanganya wawekezaji  na kuwavutiwa, kuingia  na kuendesha biashara kwa ubia ikiwemo uendeshaji a Casino nchini Malta na viwanda vya madawa  Ireland na  pia kununua  hisa kwenye Kampuni ya mafuta ya Saudi Aramco.

Alipokuwa akikutana na wawekezaji wakubwa Gignac alilazimisha apatiwe zawadi za thamani kubwa na huwakabidhi  walinzi wake wa kibiashara ambao huwatambulisha ni miongoni mwa wana ukoo wa Mfalme. 

Aikuwa akinunua beji za bandia za huduma za usalama wa kimataifa  kwa ajili ya walinzi wake na leseni za biashara za dhahabu bandia, zikiwemo kadi binafsi za biashara. Alisema mwendesha mashtaka  aliyesimamia kesi hiyo.

Ilidaiwa wakati fulani alifikia hatua ya  kutaka kununua hoteli jijini Miami miaka miwili iliyopita kwa thamani ya dola la Marekani  milion 440 na kutoa hundi ya bandia  ya Bank ya Dubai iliyompatia mkopo wa dola za kimarekani milioni 600. Jambo lililomtia shaka muuzaji wa hoteli hiyo na hatimaye kutoa taarifa Polisi

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.