Maeneo ya kuuwa watu yafichuliwa Korea Kusini

Maeneo ya kuuwa watu yafichuliwa Korea Kusini

11 June 2019 Tuesday 16:33
Maeneo ya kuuwa watu yafichuliwa Korea Kusini

Shirika moja lisilo la kiserikali nchini Korea Kusini linasema kuwa limegundua maeno 318 nchini Korea Kaskazini ambayo yanatumika na serikali kuuwa watu hadharani.

Shirika hilo limewahoji watu 610 waliotoroka Korea Kaskazini zaidi ya miaka minne iliyopita ili kuandaa ripoti yake.

Limeorodhesha mauaji yaliyotekelezwa miongo kadhaa iliyopita, ambayo yalijumuisha makosa kama ya wizi wa ng'ombe na kutizama televisheni.

Mauaji ya hadharani yalifanywa karibu na maeneo ya mtoni, viwanjani, sokoni, shuleni, na viwanja vya michezo, lilisema shirika hilo la kutetea haki.

Kundi la watu 1,000 au zaidi walikuwa wakijitokeza kushuhudia mauaji hayo, lilisema shirika hilo katika ripoti yake inayofahamika kama ''Ramani ya hatma ya waliofariki'', iliyotolewa siku ya Jumanne.

Ripoti hiyo inadai kuwa familia za wale waliohukumiwa kifo, wakiwemo watoto wakati mwingine zililazimishwa kushuhudia mauaji hayo.

Miili ya waliouawa haikuwahi kupewa familia zao wala kuoneshwa mahali ilipozikwa.

Kwa mujibu wa ushahidi, mtu mdogo zaidi kushuhudia mauaji hayo alikuwa na miaka saba.

Mauaji mengine yalikuwa yakitekelezwa katika vituo vya kuzuilia watu kama vile jela na kambi za kufanya kazi- ambapo watu walioshitakiwa kwa uhalifu wa kisiasa wanalazimishwa kufanya kazi ya ngumu kama vile ya uchumbaji madini na kukata miti.

Mmoja wa watu waliohamia kusini ambaye alizuiliwa katika kambi ya kazi miaka ya 2000 alielezea jinsi wafungwa 80 walivyolazimishwa kushuhudia mauaji ya wanawake watatu walioshitakiwa kwa jaribio la kutorokea China.

Walisema kuwa afisa wa wizara ya usalama aliwaambia watu: "Hili linaweza kuwakuta."

Ripoti hiyo inasema mauaji ni "mbinu kuu inayotumiwa na utawala kuwatia hofu wanainchi wanaojihusishana vitendo vinavyodhaniwa kuhujumu serikali".

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.