Saudi Arabia lawamani kwa kutangaza mwezi mwandamo

Saudi Arabia lawamani kwa kutangaza mwezi mwandamo

05 June 2019 Wednesday 11:56
Saudi Arabia lawamani kwa kutangaza mwezi mwandamo

UAMUZI wa Saudi Arabia   kusheherekea kumalizika kwa Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani Jumanne Juni 4, 2019, umezua tafrani kubwa kwa Waiislam huku nchi nyingi zikidai kuwa mwezi mtukufu umemalizika siku moja jioni ya kuamkia Jumatano ya Juni 5, 2019

Mwezi mtukufu wa Ramadhani humalizika baada ya kuandama kwa mwezi jambo ambalo lilithibitishwa na mamlaka ya Ufalme wa Saudi Arabia kuwa mwezi huo uliandama Jumatatu jioni. Lakini Nyaraka za kiunajimu zilibainisha siku hiyo jioni hakukuwa na uwezekano wa kuonekana kwa mwezi kwa macho kwenye eneo lolote duniani. Jambo ambalo limepunguza kuamini wa kwa wanazuoni wa Saudi Arabia

Misri nchi jirani na Saudi Arabia hawakuweza kuuona mwezi mwandamo siku ya jumatatu jioni na kuamuru wafuasi wa dini  Kiislamu kuendelea na mfungo hadi leo Jumatano Mufti Mkuu wa Misri Shawki Allam ni mtu muhimu katika hukumu mbalimbali za dini kwa dhehebu la sunni na hasa ikichukuliwa Msikiti Mkuu wa Al Azhar ndio mhimili wa dhehebu hili.

Nchi nyingine zenye Waislamu wengi za Pakistan na Indonesia nazo zimelaumu uamuzi wa Saudi kutangaza kuswali  Eid al Fitri mapema nazo pia zimeamua kuswali sikukuu hiyo leo. Utata huo umeikumba baadhi ya misikiti Jijini London kuhusiana na mwezi mwandamo. Kamati ya Uratibu wa misikiti na vituo vya kiislamu katika jiji la London hufuata mwezi mwandamo wa Saudi Arabia.

Lakini jijini Birmingham Waislamu wao wameadhimisha leo Jumatano, mjadala umewavunja nguvu wanajimu na wanakamati wa mwezi muandamo zilizoundwa na asasi za dini hiyo nchi mbalimbali, Imad Ahmed kutoka chama cha mwezi mwandamo  alisema mwezi uliotangazwa kuonekana nchini Saudi Arabia ulikuwa ni jambo lisilowezekana.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.