Waandamanaji wavamia Bungeni kushinikiza matakwa yao

Waandamanaji wavamia Bungeni kushinikiza matakwa yao

03 July 2019 Wednesday 11:11
Waandamanaji wavamia Bungeni kushinikiza matakwa yao

Hong Kong, China

BAADHI ya waandamanaji jijini Hong Kong, wameingia kwa nguvu  ndani ya jengo la Bunge la nchi hiyo, wakitishia kuvuruga shughuli za Serikali.

Hatua hiyo inafuatia maandamano ya umma kupinga sheria ambazo zitaruhusu watuhumiwa kupelekwa China kufunguliwa mashitaka. Leo ni maadhimisho ya mji wa Hong Kong kurejeshwa katika utawala wa China mwaka  1997

Maandamano hayo yamekuwa ni hatua ya moja kwa moja ya kuipinga Serikali ya China kuwa na mkono wake katika uendeshwaji wa mji huo wenye mamlaka ya ndani.

Maelfu ya wanaharakati wa kidemokrasia walifanya maandamano mengine ya amani, wakimkata kiongozi wa mji huo anayeegemea Serikali ya China kujiuzulu na kubatilisha kile wanachokiona kuwa ni miaka mingi ya kushuka kiwango cha uhuru.

Serikali ya China imelaani kitendo cha kulizingira Bunge la Hong Kong na kusema inaunga mkono kufanyika uchunguzi wa jinai dhidi ya waandamanaji waliofanya ghasia.

Hong Kong ambayo ni kitovu cha shughuhuli za kifedha na yenye mamlaka ya ndani, imekumbwa na  maandamano makubwa kwa wiki kadhaa sasa.

Waandamanaji hao wanapinga Muswada wa sheria ya kuwezesha raia wa Hong Kong kupelekwa China endapo watatakiwa kujibu mashtaka mahakamani.

Hapo juzi katika maadhimisho ya mwaka wa 22 tangu Uingereza kulirudisha jiji la Hong Kong katika mamlaka ya China, waandamani wenye misimamo mikali walivamia bunge na kuingia ndani kwa nguvu na  kutundika bendera ya enzi ya ukoloni wa Uingereza na kuchora huku kuandika vitu vya kuipinga China.

PICHANI ni baadhi waandamanaji mjini Hong Kong waliovamia Bunge la mji huo wakipinga sheria inayoruhusu kwenda kushtakiwa China.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.