banner58

Abdu Kiba yupo tayari kufanya kazi na Wasafi ya Diamond

Abdu Kiba ni ndugu wa Ali Kiba ambaye anadhaniwa kuwa na uhasama mkubwa na Diamond

Abdu Kiba yupo tayari kufanya kazi na Wasafi ya Diamond

Abdu Kiba ni ndugu wa Ali Kiba ambaye anadhaniwa kuwa na uhasama mkubwa na Diamond

02 June 2018 Saturday 13:05
Abdu Kiba yupo tayari kufanya kazi na Wasafi ya Diamond

Na Amini Nyaungo

Msanii kutoka team Kiba, Abdu Kiba amesema yupo tayari kufanya kazi na Wasafi kama anaona kuna nyimbo inahitajika akae msanii kutoka `usafini`.

Abdu Kiba ambaye ni ndugu wa Ali Kiba ambaye pia amesainiwa katika label ya Kings Music anayoimiliki Ali Kiba, amesema hakuna tatizo kumshirikisha msanii wa Wasafi kwani muziki ni ule ule.

“Muziki ni ule ule. Kama kuna haja ya kumshirikisha msanii wa WCB basi namfuata na kumshirikisha vinginevyo kama hakuna haja basi itabaki kama ilivyo. Muziki ni kama chakula, ukikipika vizuri kinakuwa kizuri. Hivyo hata nyimbo usifanye na msanii kwakuwa unafanya bali fanya ili ufanye kitu kizuri,” amesema Abdul.

Muimbaji huyo amesema mpaka sasa bado hajapata kazi ambayo anaona kuna haja ya kumtafuta msanii yeyote wa kundi hilo lilipo chini rais wa wake, Diamond Platnumz.

Abdu Kiba kupitia Kings Music ametoa ngoma tatu tayari ikiwemo ile ya `Single` aliyomshirikisha Ali Kiba huku `Jera` ambayo aliitoa kwa ajiri ya wapendanao ambao wameumizwa na nyingine ambayo ameitoa `Audio`.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.