banner68

Achana na Mr Bean muangalie Bwakila ‘Kitale’ wa Tanzania

Achana na Mr Bean muangalie Bwakila ‘Kitale’ wa Tanzania

21 May 2018 Monday 18:25
Achana na Mr Bean muangalie Bwakila ‘Kitale’ wa Tanzania

Na Amini Nyaungo

Unapotaja sanaa ya vichekesho lazima utaje jina la MR. Bean ama Charlie Chaplin kwa aina ya vichekesho vyao, huku ikisemekana ndio wenye ushawishi mkubwa kwa kipindi hiki kwa upande huo wa uchekeshaji.

Kwa Tanzania imekuwa tofauti kidogo kwa taswira iliyojengeka kuwa kuchekesha lazima uvae nguo mbaya, mfano mzuri walikuwa wanavaa nguo katika tumbo kama wana ujauzito wakati katika makalio wanavaa nguo nyingi lengo likiwa ni kuchekesha.

Inasemekana mzee Majuto ndio aliyedumu kwa muda mrefu kwa vichekesho hapa Tanzania, kuna wengine wengi wameingia katika sana hiyo ya vichekesho.

Mtu kama Mau Fundi ukimtazama tu machoni unaanza kucheka, pia wengine kama Bambo, Kingwendu, Zembwela ambaye kupitia uchekeshaji kwa sasa amekuwa mtangazaji mzuri sana akichambua vitu katika moja ya vituo vya radio nchini Tanzania.

Maswali mengi kwa kila mpenzi wa vichekesho ni kwamba, je wamenufaika kwa namna gani na Sanaa ya vichekesho?

Au ndo wakipata tatizo bakuli ihusike hayo tuwaachie.

Mussa Yusuph Kitale Bwakila ama Mkude Simba

Moja ya wasanii wa vichekesho waliofanikiwa kwa kiasi kikubwa sana hawa aina ya vichekesho vyake vinavyoendana na maisha ya sasa na utandawazi unavyotaka.

Alianza na `Kitale` akiwa kama teja amefanya vizuri baada ya hapo akaona fursa nyingine kutengeneza vichekesho vya kubishana kati ya Bwakila, Mkude Simba na Stan Bakora.

Kitale amefanikiwa sana kupitia vichekesho vyake kwani anatengeneza pesa kwa kulipwa mshahara na kuwa mwajiriwa wa E.FM.

Akimpa shavu rafiki yake Stan Bakora.

Kituo hicho kimepata wasikilizaji wengi kwa kusubiri wasikilize kichekesho chake, alinyanyua kituo hicho tangu kianze miaka minne iliyopita haswa kwa namna ya vichekesho vyake.

Watu wataweza kufikiri kuwa Bwakila na Mkude ni watu wawili tofauti, kumbe sivyo ni mtu mmoja ambaye kwa aina ya ubunifu alionao amewateka watu hadi kufikia kufikiri kuwa ni watu wawili tofauti.

Huyu Bwakila na Mkude wanamsumbua sana, ila mwisho wa siku lazima ucheke, hilo ndilo lengo lake maalumu.

Namna gani amefanikiwa angalia matangazo yalivyomfuata, kwa aina ya vichekesho vyake anatengeneza hela.

Haya ndio mabadiliko ya sanaa ya vichekesho yanavyotakiwa kwenda. Kwa hakika Kitale ndiye mshindi miongoni mwa wachekeshaji Tanzania maana inampatia pesa na burudani anatoa.

Maana halisi ya sanaa ndio hiyo kila mtu anatakiwa awe mbunifu wa aina yake ili kukuza uhalisia wa sana, kama watapatika Mkude 5 hapa Tanzania basi watainua sanaa huku wakijipatia kipato kikubwa sana.

Hapa hawajaorodheshwa kina Joti na Mpoki ambao pia wanafanya vizuri katika sanaa ya vichekesho japo hawajafika ubora wa Mkude.

Wapi anakosea

Kila kitu kina changamoto yake, tekinolojia imekuja kubadilisha kila kitu, kupitia vichekesho vyake kwa nini asiweke katika mtandao wa 'Youtube' kila kinapotoka katika radio, maana kuna watu hufaidika kwa vichekesho hivyo. Atengeneze 'Youtube Channel' aweke vichekesho vyake.

Atengengeze video fupi ili apeleke katika Television, hapa atakuwa anatengeneza ajira kwa mtengenezaji wa 'Animation' afanye kama alivyofanya katika radio hiyo itampa nguvu nyingine.

Vinginevyo ameweza na amethubutu, Azania post inampongeza sana kwa uwezo wake huu wa kuwajulia Watanzania wanataka nini.

Azania Post

Keywords:
Mkude Simba
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Kisha Kahamba 2018-05-31 23:55:04

asante.wadau ingieni youtube mtafute kisha kahamba comedy.mtaona kazi zangu

Avatar
ramadhani hassani 2018-09-05 14:40:10

uko very mdau