banner68
banner58

Ali Kiba aungana na Magufuli, adhamini kombe la dunia kwa Kiswahili

banner57

Ali Kiba aungana na Magufuli, adhamini kombe la dunia kwa Kiswahili

16 May 2018 Wednesday 15:44
Ali Kiba aungana na Magufuli, adhamini kombe la dunia kwa Kiswahili

Na Amini Nyaungo

Msanii Ali Kiba aungana na Rais John Pombe Magufuli katika kujivunia kuzaliwa katika taifa linaloongea Kiswahili.

Amesema Kiswahili ni Lugha ambayo inamtamanisha mtu akisikiliza masikioni mwake kutokana na matamshi yake, amekuwa katika safari zake nchi mbalimbali anapoongea huwa wanatamani aongee tena.

“Lazima tujivunie na Kiswahili chetu, kiswahili ni kikubwa mno watu wajue hivyo, nimekuwa natembea nchi mbalimbali wanatamani sana Lugha hii.”

“Najivunia kuongea kiswahili, najivunia kuwa mswahili, kila mtanzania anatakiwa ajivunie kuwa mswahili wala sio sifa mbaya, mtu akikuita wewe mswahili inatakiwe ufurahi, mie mswahili.”

“Najivunia pia na mimi kuwa mdhamini wa michuano hii kwa lugha ya kiswahili kinywaji changu cha Mofaya kuwa mdhamini nikishirikiana na Vodacom pamoja na Coca-cola,” amesema.

Ali Kiba alikuwepo jana na amekuwa balozi wa wa kombe la dunia kwa Lugha ya Kiswahili ambalo linarushwa moja kwa moja kupitia king`amuzi cha Star times kwenye channel za TBC 1 na TV 1 ambayo inaelekea kuchukuliwa na KWESE Sports.

Ali Kiba kupitia kinywaji chake cha Mofaya amekuwa mdhamini wa kinywaji hicho ambacho kitaanza kuuzwa rasmi baada ya mfungo wa Ramadhani wakati wa sikukuu ya Iddi.

Azania Post

Keywords:
Ali Kiba
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.